Dkt. Batilda Burhan amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga kuimarisha ushirikiano na Kenya - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 3 April 2024

Dkt. Batilda Burhan amuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga kuimarisha ushirikiano na Kenya


Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Buriani akimwapisha Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Picha na Burhani Yakub




Burhani YakubTanga.


maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Balozi Dkt. Batilda Buriani ametoa maelekezo matano kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Mkinga ya kuyatekekeza likiwamo kuimarisha ushirikiano na nchi jirani ya Kenya.


Ametoa maelekezo hayo mapema leo wakati akimwapisha Gilbert Kalima kuwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Mkinga.


Kilima anachukua nafasi ya Evance Alfread Mtambi ambaye  Machi 2 mwaka huu  aliapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na juzi akapata uteuzi wa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.


Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali Mkoani hapa, Dkt. Batilda amesema kazi ambayo inamkabili Kalima ni kushughulikia changamoto ya migogoro iliyopo Wilayani Mkinga.


"Mkinga ni miongoni mwa Wilaya zenye migogoro katika mkoa wetu, nenda kahakikishe unaitatua ili iweze kumalizika na wananchi waweze kuishi kwa amani"amesema Buriani.


Jukumu jingine ni kwamba Wilaya ya Mkinga ina utajiri wa uchumi wa buluu kupitia bahari ya Hindi kwa hivyo atumie nafasi yake kuwawezesha wananchi kunufaika kiuchumi kupitia fursa hiyo.


"Kaache alama kwa kuibua kwa kuibua fursa za uchumi wa buluu, kupitia uvuvi, ufugaji wa majongoo bahari, kilmo cha mwani na kaa wa baharini"amesema Buriani.


Amemuagiza pia kusimamia suala za lishe kwa watoto wa  Mkinga ili kukuza kizazi chenye afya bora huku akimsisitiza kuwa Mkinga ni Wilaya iliyopo mpakani na ni njia ya mapito ya wahamiaji haramu na upitishaji wa dawa za kulevya na bidhaa za magendo.


"Lakini pia kuna mambo mtambuka kama uhifadhi wa mazingira na kusimamia kutopandishwa kiholela bei za bidhaa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu ya Idd El Fitri"amesema Buriani.


Kuhusu mahusiano na nchi jirani ya Kenya, Mkuu wa Mkoa amesema Mkinga ni Wilaya iliyopo mpakani huvyo kunahitajika kuimarisha mahusiano baina ili wananchi wa Pande zote waendeshe shughuli zao bila.


Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga,Kalima alikuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.


Akizungumzia baada ya kuapishwa, Kalima ameahidi kutekeleza maelekezo ya Mkuu wa Mkoa lakini ameomba ushirikiano na viongozi pamoja na wananchi wa Wilaya hiyo.


No comments: