NAIBU KATIBU MKUU BARA JOHN MONGELA ASEMA UNYONGE CCM SASA BASI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 5 April 2024

NAIBU KATIBU MKUU BARA JOHN MONGELA ASEMA UNYONGE CCM SASA BASI




Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella akizungumza na wanaccm wa Daresalaam 




Na: Mwandishi wetu, DSM

maipacarusha20@gmail.com

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Mongella amewataka Wanachama wa CCM wajiamini huku akisema kumekuwa na maeneo Wana CCM wanatishwa kitoto ambapo amewataka wasikubali kutishwa na yeyote.


Ndugu. John Mongella akiunguruma kwa kutoa salamu za shukrani kwa Mapokezi mazuri na makubwa kutoka kwa Viongozi mbalimbali wa Chama , Jumuiya na Serikali, Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa CCM yaliyofanyika leo tarehe 5 Aprili, 2024 katika kiwanja cha nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam, Lumumba




“Mimi kwa nafasi yangu kama Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara sio Mtu wa majukwaa sana, niwaahidi nitasimamia kuhakikisha utendaji ndani ya Chama chetu unaakisi ukubwa wa Chama, kama Mtu ana akili timamu baada ya kumsikia Jokate, Ally Hapi, Makalla maana yake muziki umeanza na Mimi nataka kusema kama kuna Mtu alikuwa hamuelewi vizuri Mh. Rais Dkt. Samia hii safu ni ujumbe tosha”.Amesema Mongella




“Kazi yetu ni kujipanga na Wana CCM tuwe na kujiamini, kuna maeneo Wana CCM wanatishwa kitotototo, tusikubali kutishwa na yeyote, Mimi nakumbuka tulipiga marufuku Watu kutishwa hapa Mjini ilikuwa marufuku Watu kutishwa Mtu akitaka aje kistaarabu, Vijana lazima tusimame kukilinda Chama”.Amesema Mongella.




“Na mmepata Katibu Mkuu imara, Mwenyekiti imara, Viongozi imara, UVCCM mna jukumu la kulinda Viongozi wa Chama na mali za Chama, wote tuna Dini zetu na Madhehebu yetu lakini CCM sio Dhehebu ina kazi ya kutafuta Dola, kwahiyo katika kushika Dola hakuna kubembelezana”. Amesema Mongella.




“Hakuna Shangazi wala Mjomba, tukimaliza kushika Dola Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu tutakuja tutakaa mezani tutakunywa kahawa, na jambo hili wala halina mzaha lakini kama wenzangu walivyosema Mh. Rais ni Muumini wa maridhiano na mapatano na demokrasia ya kweli”. Amesema Mongella.




“Tungeomba wote uwe mwelekeo wetu mpaka Vyama rafiki, lakini pale Mtu akikata kwenda vinginevyo sisi huku hasa kwenye Sekretarieti hii utaalamu upo wa kutosha wa hayo mengine lakini tutakuwa Wavumilivu kwasababu Mwenyekiti wa Chama chetu anaamini katika hilo lakini ushindi wa CCM ni lazima wala halina mjadala”. Amesema Mongella.









No comments: