CHANGAMOTO YA WANAFUNZI KUKAA CHINI MBUNGEABOOD AKABIDHI MADAWATI YA THAMANI YA SH, MIL. 28 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 14 May 2024

CHANGAMOTO YA WANAFUNZI KUKAA CHINI MBUNGEABOOD AKABIDHI MADAWATI YA THAMANI YA SH, MIL. 28

 







Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


Madawati yenye thamani ya zaidi ya sh. Mil. 28 yamekabidhiwa katika Shule ya Sekondari ya Mazimbu iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz Abood.


Madawati hayo yamekabidhiwa kufuatia ziara ya Mbunge huyo kutembelea na kukagua maendeleo ya Shule mpya zilizojengwa katika Halmashauri hiyo kwa kutumia nguvu za wananchi, fedha za mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali kuu, maarufu kama fedha za Uviko 19 na kuona changamoto ya wanafunzi kukaa chini hivyo kuahidi kupeleka viti na meza kwenye Shule hiyo.


Zoezi hilo la kukabidhi madawati katika Shule hiyo limefanyika kufuatia ziara ya Mbunge Abood alioifanya Januari 10 Mwaka huu kwenye Shule hiyo na kujionea upungufu mkubwa wa Madawati pamoja na Viti, ambapo kwa kiasi kikubwa aliona namna wanafunzi wa Shule hiyo Mpya wanavyokumbana na changamoto ya kukaa chini.


Aidha ili waweze kujifunza kwa utulivu na hiyvo, kuamua kupeleka Madawati hayo ambayo ni Meza 310 pamoja na viti 310 ili kuondoa changamoto hiyo.


Abood aliweka wazi kuwa, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika kuimarisha miundombinu ya elimu kwa kuendeleza ujenzi wa Shule za Sekondari na Msingi nchini kote ili elimu yenye ubora iweze kutolewa kwa kiwango chenye uhakika na hatimaye Taifa liweze kushindana na kuendana na vigezo vya ushindani katika soko la ajira.


Aidha,Abood alifafanua kwamba, ujenzi wa madarasa ni jambo moja na kuunga mkono jitihada za  Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka madawati ili watoto waweza kupata hari ya kusoma ni jambo lingine.


Alisema kama Mbunge aliona hilo na kuamua kutengeneza Meza pamoja na Viti vyenye uwezo wa kutosha kuhudumia wanafunzi na madarasa zaidi 6, kwa lengo la kuwafanya walimu wafundishe vyema na wanafunzi wajifunze kwa utulivu mkubwa na kuleta matokeo chanya ya kielimu kwenye Manispaa hiyo na Taifa kwa ujumla.


“Nilikuja hapa katika ziara yangu ya kushtukiza na nikakutana na changamoto ya madawa,"alisema.


Baadhi ya wananchi walipongeza jitihada za Mbunge huyo kwa namna anavyosaidia wananchi kwenye masuala mbalimbali pamoja na taasisi.


Halima Rashid mkazi wa Manispaa ya Morogoro alisema Abood amekuwa akisaidia watu wa mahitaji maalumu, wanafunzi, shule, pamoja na Hospitali.



No comments: