MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO KUTOFURAHISHWA NA KUZAGAA KWA TAKA OVYO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 16 May 2024

MADIWANI MANISPAA YA MOROGORO KUTOFURAHISHWA NA KUZAGAA KWA TAKA OVYO

 

Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga akizungumza katika mkutano wa Baraza la madiwani.


Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro Fadhili Chilombe


Na Lilian Kasenene, Morogoro.

maipacarusha20@gmail.com


Baraza la Madiwani la Manispaa ya Morogoro limeeleza kuwa kila kinachotokea ndani ya Manispaa ya Morogoro limekuwa likikiona ikiwemo kutofurahishwa na suala la kuzagaa ovyo kwa tak.


Kwamba kama madiwani wamekuwa na mijadala mirefu juu suala hilo la takataka na kulazimika kuomba kuongezwa kwa bei ya uzoaji taka hizo.


Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga alizungumza hayo wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za robo ya tatu ya Januari hadi Machi mwaka 2024 


Kihanga alisema baraza baada ya majadiliano wameomba kuongezwa kwa bei ya uzoaji wa taka na tayari serikali imeleta bei hizo na zitaanza kutumika baada ya kupitishwa.


“Tunatamani mjii huu uwe msafi na uweze kuongoza, kama kweli bei hizi zitawalipa wakandarasi tukiona kuna uchafu tutawashughulikia wao na hatutarajii baadaya mchakato anaoendelea nao mkurugenzi kuona tena mrundo ya taka hatutarajii,”alisema.


Akitoa salamu za Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Morogoro mjini, katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wilaya hiyo Sabrina Juma ambaye alikaribishwa kwenye mkutano huo,alisema chama kimekuwa na mambo kadhaa ya kuwasemea wananchi ambayo yamekuwa yakilalamikiwa ni kuharibika kwa barabara za ndani na kuwa uchkavu,Maji kuwa changamoto,pamoja na kuishi kwa ushirikiano.


Alizungumzia suala la Uratibu wa uzoaji wa takataka ndani ya manispaa ya morogoro akikitaka kikao hicho baraza kutatua changamoto hiyo ili kuleta majibu na muafaka kwa wananchi ili kuondoak malalamiko yaliyopo.  


Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa wiaya ya Morogoro Rebeca Nsemwa alisema ni wajibu wa madiwani kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi yote iliyotekelezwa katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa wataalamu wa Manispaa hiyo endapo kuna changamoto yoyote.


“Tunatamani ifikapo mwisho wa 2024 kila kitu kiwe kimekamilika, tuna kila sababu ya kufanya vizuri kwani mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kipaumbele sana kwenye masual yote muhimu kama Afya, na Elimu tuna miradi ya kutosha,”alisema.


Aidha alisema bado kumekuwa na suala la ukatili dhidiya wananwake na watoto umekuwa ukiendelea kwenye maeneo ndani ya manispaa ya Morogoro ambapo alieleza kuwa anatamani kutafuta namna ya kuandaa utoaji wa elimu kwa jamii na familia.


Akawaomba madiwani kuhakikisha kwenye vikao vyao vya kata kuweka ajenda mahususi ya kukemea ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kuwatumia maafisa ustawi wa jamii katiiamkutoa elimu kwani hali si shwari sana.


Katika kikao hichomcha baraza alikaribishwa Meneja wa shirika la Umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Morogoro Mhandisi Fadhili Chilombe alieleza kuwa kumekuwa na changamoto kadhaa ambayo imekuwa ikitokea ndani ya mkoa wa Morogoro ikiwemo wananchi kuuziwa fomu jambo ambalo si sahihi kwani fomu hiyo ni bure akawaomba madiwani kuwaeleza wananchi wao.


Mhandisi Chilombe alisema mambo mengine yametokea ambayo Tanesco imeendelea kuyasimamia kwa karibu ikiwemo baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu kuwaomba wateja fedha ya mafuta na kuwaomba kushirikiana kuwafichua na baadhi wamechukuliwa hatua kutokana na kuichafua serikali na shirika.


Meneja huyo alisema Tanesco katika kipindi cha Mafuriko mambo mengi walikutana nayo na ghalama zilizoghalamiwa kutokana na uhalibifu nii sh 139 milioni kwa mkoa mzima, na kwamba kwa mtu mmoja mmoja waliotoa taafisa za kukosa umeme kwa maana ya malalamiko kwa kipindi hicho cha mafuriko ni watu 800.


Aidha alisema Tanesco imekuja na mpango mpya wa kuitengeneza Morogoro mpya kwenye Umeme kwa kuondoa miundombinu mibovu ya zamani, kuondoa waya zote zisizokuwa na kava,kuweka nguzo za Zege ambapo baadhi ya maeneo yameanza kufanyika kama Kingolwira,Kiwanja cha Ndege, na kwamba katika kutatua matatizo hayo kuna maeneo yamekuwa korofi na kufanya kukatika umeme kila siku.


Pia alisema kumekuwa na changamoto ya wizi wa miundombinu ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya hujuma kwa kuiba transfoma, waya,mafuta na hiyo imeleta kero kwa wananhi na hasara kwa serikali.


Mkurugenzi wa Mansiapaa hiyo ya Morogoro Emmanuel Mkongo akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa diwani kata ya Mjimpya Emmi Kihula ambaye alitaka kufahamu kuwa standi ya Mafiga imekuwa haina sehemu ya kujihifadhi kwa Mvua na Jua kwa watoa huduma wanaotoa risiti kwa abiria na magari yanayotoka kwa maana ya uwepo wa ofisi, Manispaa inachukua hatua gani kuhakikihsa panakuwepo na ofisi hiyo wawe kwenye hali salama.


“Tumepokea hoja ya mheshimiwa Kihula na tutaifanyiakazi na kuipitisha kwenye kamati hususani kamati ya fedha ili kuondoa changamoto hiyo kwa haraka,”alisema mkurugenzi Mkongo.


No comments: