WANAHABARI TANGAZENI UTALII WA MOROGORO KWANI NI KITOVU CHA UTALII - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 11 May 2024

WANAHABARI TANGAZENI UTALII WA MOROGORO KWANI NI KITOVU CHA UTALII

 

MKUU wa Mkoa Morogoro Adam Malima (katikati) akifungua Mafunzo kwa wanahabari yaliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa habari Tanzania (TAMPA) kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), kushoto ni Katibu wa Chama Cha waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro (MoroPC) Lilian Kasenene na kulia ni Rais wa TAMPA, Simon Mkina 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mkoani Morogoro mara baada ya kufunga mafunzo



Na: Mwandishi wetu, Morogoro

maipacarusha20@gmail.com


MKUU wa Mkoa Morogoro Adam Malima amewataka wanahabari kuwa mabalozi wa utalii, kuandika taarifa zinazowavutia watalii kutoka  ndani na nje ya nchi.


RC Malima ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo kwa wanahabari yaliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa habari Tanzania (TAMPA) kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa(TANAPA)


Alisema Mkoa wa Morogoro unahifadhi Tatu Kubwa ambazo ni Mikumi, Udzungwa na Mwalimu Nyerere zenye vivutio kadha wa kadha huku vingine vikiwa havipatikani mahala popote Duniani


"Katika kutoa fursa kwa watalii kuweza kufika kwa urahisi katika hifadhi ya Taifa Mikumi serikali ina mpango kufungua geti Kilosa kuingia Hifadhi hiyo kutokana na kuwepo kwa treni ya mwendokasi(SGR).


Alisema kwa Sasa watalii wanalazimika kusafiri zaidi ya kilometa 100 kutoka Kilosa mjini hadi Mikumi na endapo geti hilo litafunguliwa watasafiri kilometa 15 kuingia hifadhini.


Alisema hifadhi ya Mikumi inafikika kwa urahisi kwa kutumia njia mbalimbali ambazo ni barabara ya TAZAM, Reli ya kati, Reli ya SGR na njia ya anga hivyo watalii wanapata fursa ya kuona wanyama kirahisi.


Aidha mkuu huyo wa mkoa Malima aliwataka wadau mbalimbali kuanza kujenga hoteli nzuri zenye viwango katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kisaki ili kuhudumia watalii wanaotembelea hifadhi ya Mwalimu Nyerere, Mikumi, Doma kwa hifadhi ya Mikumi na Ruaha kwa hifadhi ya Udzungwa.


Akizungumza katika mafunzo hayo Rais wa TAMPA, Simon Mkina alisema lengo la semina hiyo ni kuwaandaa wanabari kuwa sehemu ya utalii Kwa kushiriki moja kwa moja Ili kutimiza malengo ya Serikali kupitia filamu ya THE ROYAL TOUR.


Naye Katibu wa Chama Cha  waandishi wa Habari mkoa wa Morogoro (MoroPC) Lilian Kasenene alisema mafunzo hayo yametolewa muda muafaka ambapo ameahidi kuwa chama hicho kupitia wanachama wake kitakuwa mstari wa mbele katika kitangaza utalii wa Morogoro.


Naye Mkufunzi Mwanadamizi Chuo cha Taifa cha Utalii Agapiti Roman alisena mwaka 2023 jumla ya watalii Milioni 1.8 walitembelea Hifadhi za Taifa nchini kutoka Milion 1.3 mwaka 2022 na hii ni ongezeko kubwa baada ya filamu ya THE ROYAL TOUR ambayo imekua chahu kubwa kwa nchi.



No comments: