WATU WANNE WAFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI MGODINI WILAYANI ULANGA MKOANI MOROGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 10 May 2024

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI MGODINI WILAYANI ULANGA MKOANI MOROGORO

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama akizungumza na waandishi wa habari 


Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipac20@gmail.com


WATU wanne wamefariki Dunia na  wengine wanne kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa Alcaeda uliopo kata ya Nawenge wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.


Akizungumza na Waandishi wa Habari,Kamanda wa polisi mkoani hapa Alex Mkama alisema tukio hilo limetokea Jana wilayani humo baada ya kifusi hicho kudondoka na kuwafukia watu hao na kusababisha vifo vyao.


Kamanda huyo aliwataja waliofariki kuwa ni Shiwa Kadege(30) mkazi wa Tabora, Ismail Bashiru (35) mkazi wa Arusha , Steven Mpiondi (34) mkazi wa Ulanga na Shaban Andrea   (34) mkazi wa Masasi.


Alisema miili ya Marehemu hao imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Ulanga ikisubiri taratibu za  huku majeruhi walitibiwa na kuruhusiwa.


Alisema chanzo cha tukio hilo ni watu hao waliingia ndani zaidi katika mgodi huo ambapo udogo ulimeguka na kuwafukia watu 8 ambaoo wanne kati yao walifanikiwa kuokolewa.


" Watu hawa wanatoka sehemu mbalimbali hapa nchini kwenda katika mgodi huo kuchimba madini, sasa kufutia mvua hizi zinazonyesha ndio udongo ukameguka na kuwafukia"alisema.


Alisema uchunguzi unaendelea kwa kuwashirikisha idara ya Madini na Uhamiaji ili kubaini uhalali wa mgodi huo kama upo kihalali au laa.


Mkama alieleza kuwa jeshi hilo linafanya pia uchunguzi tukio la vifo vya watu wanne vilivyotokea katika mgodi huo.


Kamanda Mkama alieleza kuwa Watu hao walidondokewa na ngema ya mgodi huo na kufunikwa na kifusi kilicho sababisha umauti wao na majeruha.


"Bado tunafanya uchunguzi,tukio limetokea Jana tunafanya uchunguzi ili kujua Kwanza kama mgodi huu upo kihalali na kilichotokea ni kwamba kuna baadhi ya wachimbaji wanaenda mpaka underground na sahivi Mvua zinaendelea kunyesha ardhi haijajishika vizuri unapotokea mtikisiko wowote ule lolote linaweza kutokea,"alisema.


"Kwa hiyo udongo ulijimega na kuwafunika waliokua chini na kusababisha kukosa hewa na kukutwa na umauti lakini tumeokoa wengine wanne".alisema Kamanda Alex.


Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ruby International limited Katika mgodi wa Epanko Betold Matambala alieleza kuwa ajali hiyo ilisababishwa na kumegeka kwa mwamba na kusababisha Vifo hivyo huku akikanusha kuwa ajali hiyo haikusababishwa na Mvua zinazoendelea.


Mkurugenzi huyo alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa kumi jioni na kusema kuwa shughuli hizo hutekelezwa Kwa kutumia vilipuzi hivyo kulitokea mtikisiko na kusababisha jiwe kumegeka na kuwafunika wachimbaji hao.


No comments: