MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima |
Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amewataka madiwani na watendaji wa Halmashauri ya Mlimba, Wilayani Kilombero,mkoa wa Morogoro kufanya kazi za kuletea maendeleo kwa wananchi na kuhamasisha shughuli za uzalishaji wa mazao ya kimkakati yatakayochangia kuongeza mapato yao na ya halmashauri kwa ajili ya kuboresha huduma za kijamii.
Hatua hiyo inatokana na wakulima wa zao la kokoa katika Halmashauri hiyo kuanza kufaidika baada ya kufanyika mnada wa kwanza wa ununuzi wa kwa njia ya mtandao uliowaingizia fedha kiasi cha Shilingi bilioni 1.1.
Katika mnada huo jumla ya kilo 43,750 za Kakao ziliuzwa kwa bei ya Sh 25,720 kwa kilo, kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani unaoratibiwa na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
Malima alisema hayo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kujadili hoja sita za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa halmshauri hiyo .
Alisema halmshauri ya Mlimba kimsingi ni ya kilimo na mapato yake yanategemea mazao ya kilimo yaliwemo ya mpunga, ndizi na kokoa hivyo madiwani na watendaji wanaowajibu kusimamia Maendeleo.
“ Bahati nzuri wiki iliyopita nilikuwa Mlimba na kulikuwa na mnada wa zao kakao uliokusanya tani 43 na zikapatikana Sh bilioni 1.1 na katika hilo fedha iliyoenda halmashauri ni Sh milioni 33” alisema Malima .
Malima alisema , halmashauri hiyo ya Mlimba kutokana na kuwepo ardhi yenye rubuta na inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo ya kimkakati ambayo inauwezo wa kuongoza kimapato kimkoa na kuchangia kuongeza kipato cha mwananchi na pia kwa halmashauri .
Alisema kuwa ,madiwani kwa kushirikiana na watendaji wa halmashauri hiyo wakiweka mkazo kuhamashisha uzalishaji wa zao la kokoa kwa hatua za awali itaweza kuzalisha tani 1,000 kwa mwaka zenye thamani ya Sh bilioni 900 na halmashauri kujipati mapato ya zaidi ya Sh bilioni 4 endapo juhudi hizo zitaongezwa upo uwezekano wa kufikia zaidi ya tani 5,000 wa mwaka.
" Halmashauri hii ya Mlimba inaweza kujiendesha Kwa kokoa tu endapo uzalishaji ukaongezeka mara dufu" alisema Malima.
Mkuu wa mkoa pia aliwatahadharisha madiwani wanaopingana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu matumizi ya mfumo wa Stakabadhi Gharani ya wanajiweka katika mazingira magumu.
“Diwani lazima muwe na wivu wa maendeleo , Diwani ujiulize mimi ni diwani maendeleo au diwani maslahi nah ii pia kwa watendaji mjiuliza mimi ni mtendaji maendeleo au mtendaji maslahi” alisisitiza Malima.
Pamoja na hayo mkuu wa mkoa aliasihi madiwani na viongozi wengine kuacha mara moja kuanzisha migogoro isiyo na tija , bali waelekeza nguvu zao katika kusimamia miradi maendeleo ya wananchi na utoajiwa huduma bora.
Naye Mkuu wa Wilaya Kilombero , Dunstan Kyobya alisema halmashauri hiyo alizindua mnada wa zao kokoa na bei ya Sh 25, 720 ambayo haujawahi kutokea na ulifanyika katika ghala la Chama cha Msingi cha Wakulima (AMCOS) lililopo kata ya Mbingu, Mlimba.
Alisema fedha ambayo kwa mujibu wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), inaingizwa moja kwa moja kwenye akaunti za wakulima na akaunti ya Halmashauri hiyo.
Kyobya alisema wanaendelea kuwahimiza wananchi kuongeza bidii katika kilimo cha mazao ya kimkakati kakao, karafuu, michikichi , kahawa, pamba na ufuta.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo , Innocent Mwangasa alisema ,halmashauri yao imekuwa ni ya kuingwa ndani ya halmashauri zote za mkoa huo ikiwemo ya ukusanyaji wa mapato imekuwa ikishika nafasi ya kwanza , usimamizi wa miradi na sekta ya elimu.
Halmashauri hiyo imepata hati safi inayoridhisha kwa miaka mitano mfululizo na katika kikao hicho jumla ya hoja sita zilijadiliwa na zimepewa muda wa kukamilishwa ili ziweze kufutwa na CAG.
No comments:
Post a Comment