Na:Mussa Juma,Maipac
maipacarusha20@gmail.com
Wadau kutoka sekta mbalimbali nchini,wakiongozwa na mtandao wa watetezi wa Haki za Binaadamu (THRDC)leo wamekutana jijini Dodoma kwa lengo la kutoa maoni yao na mapendekezo juu ya muswada wa Fedha wa mwaka 2024 - (Financial Bill 2024).
Viongozi wa Asasi wakiongozwa na mratibu wa Taifa wa THRDC,Onesmo Ole Ngurumwa
Licha ya kutoa maoni kadhaa kuboresha muswada huo pia wametoa pongezi kusikilizwa kilio cha AZAKi.
AZAKi pia zimeipongeza Wizara ya fedha kwa kukubali baadhi ya mapendekezo ya AZAKI ya muda mrefu kuhusu kurekebisha kifungu cha 64 cha Sheria ya Mapato ya Kodi kwa kupanua tafsiri ya Shirika la Hisani ( charitable organization) na kuongeza tasisi za afya na mazingira.
Ole Ngurumwa alisema , ingawa maboresho haya ni madogo kulingana na mapendekezo ya AZAKi yaliyotaka kugusa maeneo yote yanayofanyiwa kazi na AZAKi kama msaada wa kisheria , Elimu , kupambana na ukatili wa watoto , utawala bora , haki za binadamu lakini walau kuna maboresho.
Wengine waliowasikisha maoni ni pamoja na Musa Jonasi - Mwakilishi wa katibu Nacongo na Charlotte Kabunga -mwakilishi THRDC kanda ya kati .
"Tumekuja kushiriki katika Mkutano huu kwa ajili ya kutoa uchambuzi uliofanywa juu ya mswada huu, namna unavyoweza kuathiri uendeshaji wa shughuli mbalimbali za mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) hasa za kifedha na kikodi katika kutekeleza malengo za AZAKI "alisema ole Ngurumwa
Amesema lengo la mapendekezo yao ni uboreshaji wa mswada huu kwa manufaa Mashirika yasiyo ya kiserikali na ya taifa kiujumla.
"Tumewasilisha pendekezo kwa kamati namba ya kuboresha tafsiri ya asasi ya hisani hapa nchini"alisema
THRDC kupitia wanachama wake Kila mwaka wamekuwa wakifanya uchambuzi wa bajeti,masuala ya Kodi na sheria mbalimbali ili kuboresha Utendaji wa AZAKi kwa manufaa ya umma.
No comments:
Post a Comment