ASASI NDOGO ZA FEDHA WEKENI WAZI MASHARTI YA UKOPESHAJI KUEPUKA MALALAMIKO, Wakurugenzi wa Asasi 55 wafikiwa Morogoro na Mfuko wa Self kupata elimu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 1 July 2024

ASASI NDOGO ZA FEDHA WEKENI WAZI MASHARTI YA UKOPESHAJI KUEPUKA MALALAMIKO, Wakurugenzi wa Asasi 55 wafikiwa Morogoro na Mfuko wa Self kupata elimu






Na Lilian Kasenene, Morogoro 


maipacarusha20@gmail.com


WAKURUGENZI na wasimamizi wa asasi ndogo za fedha mkoa wa Morogoro wametakiwa kuweka wazi gharama, na masharti ya ukopeshaji wa fedha kwa wateja wao ili kuepuka malalamiko yanayojitokeza kwa sasa kwa watoa huduma hao.


Meneja wa Mfuko wa Self Mkoa wa Morogoro Moses Ntambi alieleza hayo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi na wakurugenzi wa asasi hizo ndogo za fedha yanayotolewa na Mfuko huo uliopo chini ya Wizara ya Fedha yenye jukumu la kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali na kutoa mikopo nafuu kwa wananchi.


Ntambi alisema asasi ndogo za kifedha zinazotoa mikopo kwa wajasiliamali,wananchi na taasisi mbalimbali zinatakiwa kuwa na masharti nafuu kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni zilizowekwa na Banki kuu ya Tanzania (BoT) na kwamba mkuko huo wa Self unatoa elimu ya fedha na utoaji wa mikopo nafuu kwa asasi hizo ambapo asasi 55 zilizosajiliwa Morogoro zimepatiwa mafunzo.


“Nia ya kuwakutaniasha na kuwajengea uwezo masuala ya usimamizi wa fedha, ingawa katika kundi hili kuna taasisi zina uzoefu wa muda mrefu na kuna nyingine bado ni changa tangu kuanza kwa biashara hii kwa hiyo wote tunawapa elimu ili waweze kutoa huduma jinsi inavyostahili kutokana na maelekezo na sheria,”alisema nNtambi.


Alisema mkoa wa Morogoro kwa kipindi cha miaka miwili umeweza kutoa mikopo kwa zaidi ya bilioni 4 kwa taasisi 18 na fedha zote zimewafikia watu mbalimbali wakiwemo wajasiliamali,wakulima,asasi za fedha mbalimbali na wenye viwanda vidogo.


Ntambi alisema mafanikio yaliyopatikaana ni pamoja na kuongeza ajira hususani kwa vijana na kuona usigawi wa biashara za watu waliowakopesha na ustawi wa uchumi wa kibiashara na maisha binafsi.


Akizungumzia suala la mikopo umiza alisema wameendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi ambapo wamekuwa na makongamano, na kwamba mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha kwenda kwa wananchi lazima ghalama zake ziwe wazi ili mteja aweze kukubali ana kukataa kukopo kwa hiari yake.


Meneja huyo wa mfuko wa Self alisema changamoto wanayokutana nayo ni pamoja na mkopaji kutotimiza lengo alilopewa mkopo na kuaacha kufanyia uzalishaji, jambo linalosababisha mkopo kutolipika kwa wakati,


Katibu wa Umoja wa wakopeshaji Tanzania wasiochukua Amana(TAMIU) Wambura Mirumbe alisema mafunzo hayo ni chachu ya kufanya kazi ya ukopeshaji kwa weledi, makini na kwamba hiyo itawezesha kumuhudumia mwananchi bila kuwa na makndokando na kuondoa malalamiko kwao nankuwepo kwa ustawi.


Aidha Mirumbe alisema mwananchi anapotarajia kukopa ni vyema akajua taratibu, masharti na vigezo vyote vinavyohitajika pamoja na kujua mpoko anaouchukua ni kwa ajili ya lengo mahususi ili kuondokana na kuchukuliwa bidhaa ama dhamana yake bila sababu.


Naye Meneja Masoko na Uhamasishaji Mfuko wa Self Linda Mshana alisema baada ya kuona uwepo wa umbali baina ya taasisi zinazotoa mikopo kwa kukosa maarifa kamili kwa ajili ya kufanya kazi kikamilifu,ndipo mfuko ukaamua kuanza kutoa elimu hiyo ili kusaidia wananchi.


Pia alisema mikoa 12 itafikiwa na kwamba mpaka sasa mikopo iliyotolewa ni shilingi bilioni 314 na wateja zaidi ya 200,000 wamefikiwa kwa nchi nzima na matarajio yake ni kuwafikia wengi zaidi.


Mfuko wa Self ni taasisi ya kiserikali iliyo chini yaWizara ya Fedha.


No comments: