DC ATOA SIKU TATU MKANDARASI KULIPA DENI LA MIL 46, AWATAKA WANANCHI KURUDISHA MALI WALIZOCHUKUA. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 2 July 2024

DC ATOA SIKU TATU MKANDARASI KULIPA DENI LA MIL 46, AWATAKA WANANCHI KURUDISHA MALI WALIZOCHUKUA.














Na: Lilian Kasenene, Morogoro




maipacarusha20@gmail.com


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli amemtaka aliyekuwa Mkandarasi wa ujenzi wa kisima cha maji katika kitongoji cha Sokoine Ranchi kulipa deni la zaidi ya sh milioni 46 anayodaiwa na vibarua, mama lishe pamoja na mzabuni.


Nguli alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Sokoine Ranchi alipotembelea baada ya kupokea malalamiko ya wananchi juu ya Mkandarasi huyo.


Mkuu huyo wa Wilaya alisema Mkandarasi uyo anatoka kwenye kampuni Selflink limited ambaye inadaiwa ni ya mtumishi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Rukwa.


Kwa mujibu wa mkataba Mkandarasi huyo alishalipwa asilima 90 ya kazi lakini kwa sasa amesimamishwa kuendelea na ujenzi huo.


Aidha,Nguli alubainisha kuwa jitihada mbalimbali za kumtafuta zimefanyika ili alipe madeni yake lakini mkandarasi huyo hajajitokeza mpaka Sasa.


"Nimpe siku tatu huyo msimamizi wa mradi na kampuni yake siku tatu kuyalipa madeni yake mara moja nia ni wananchi wapate huduma," alisema Mkuu huyo wa Wilaya.


Sambamba na hilo Judith Nguli aliwataka wananchi kurudisha mali za mkandarasi walizochukua ikiwemo vifaa vya mradi pamoja na gari aina ya Toyota Nissan lenye namba za usajiri T 471 AMK na kuwataka kutojichukulia sheria mkononi.


Kwa upande wao vibarua wanaomdai mkandarasi huyo akiwemo Juma Daniel alisema alipewa kazi ya kuchimba karo la tenki la maji ambapo malipo yake ni sh 290,000 lakini hadi sasa amelipwa sh 150,000 tu.


Naye Halima Seluhinga alisema aliwapangisha chumba kwenye nyumba ya wageni ambapo pesa anayodai ni sh 500,000, flemu ya duka sh 70,000 na baadhi ya vyombo vimechukuliwa na wafanyakazi wa mkandarasi huyo.


Aidha, alibainisha kuwa aliamua kulizuia gari la mkandarasi hadi pale atakapolipwa lakini kwa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya anarudisha gari hilo.

No comments: