DC Kaganda Atoa Wiki moja Kukamilishwa kwa Jengo la Mama na Mtoto kituo Cha Afya Bashnet - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 10 October 2024

DC Kaganda Atoa Wiki moja Kukamilishwa kwa Jengo la Mama na Mtoto kituo Cha Afya Bashnet

 








Na Epifania Magingo Babati, Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Wilaya ya Babati Mji Emmanuela Mtatifikolo Kaganda ametoa wiki moja kukamilika kwa jengo la huduma ya mama na mtoto lililopo katika Kituo cha Afya cha kata ya Bashnet ili kuwasaidia kina mama waweze kupata huduma kwa urahisi na kuepuka kutembea umbali mrefu kwenda kwenye vituo vingine.


Ametoa agizo hilo wakati alipotembelea kituo cha Afya cha Bashnet ili kujionea maendeleo ya mradi huo wa Kituo cha Afya ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoifanya kwenye kata ya Bashnet iliyopo Wilayani Babati, na kugundua kuna uzembe mkubwa katika ukamilishaji wa jengo hilo baada ya kupata taarifa kuwa fundi aliyekabidhiwa kujenga kutofika 

eneo la kazi kwa wakati na kupelekea mradi kuchukua mda mrefu kukamilika.

 

“Ninawapa wiki moja kufanya kazi, afya za wananchi ni kipaumbele chetu, kama hela ipo na kilakitu kipo sasa nataka nijue nani anakwamisha, kama hadi kina mama wanalalamika mliwaahidi mwezi wa nane lakini hadi leo hamjakamilisha nyie mnajisikiaje?”


Aidha , Mkuu wa Wilaya amesisitiza kuwa hawatofumbia macho jambo lolote linalokwamisha miradi ya maendeleo na lengo kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ikiwemo za Afya ili kuwa na Taifa lenye Afya njema hasa huduma ya mama na mtoto kama ilivyo kipaumbele cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


“Tutaweka mkazo na msisitizo ili huduma iweze kupatikana ili lile lengo la mheshimiwa Raisi wa jamhuri ya muungato wa Tanzania la kuhakikisha kwamba tunakuwa na vifo sifuri vya mama na mtoto, hivyo tutapambana kuhakikisha mnaipata huduma hiyo kwa haraka.”


Awali,akizungumza na baadhi ya wakina mama waliokwenda  kupata huduma katika kituo hicho  cha Afya  cha Bashnet wananchi hao wamesema imekuwa kero kubwa kwao kwani ahadi ya kukamilika kwa jengo la huduma ya mama na mtoto imekuwa ya muda mrefu tangu mwezi wa nane, hivyo wakaiomba serikali iwasaidie kukamilisha jengo hilo ili wakina mama waanze kupata huduma.

No comments: