DC KAGANDA ATUMIA BAJAJI KUHAMASISHA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 15 October 2024

DC KAGANDA ATUMIA BAJAJI KUHAMASISHA UANDIKISHAJI WAPIGA KURA

 





Na Epifania Magingo, Manyara 


Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda  amelazimika kutumia usafiri wa pikipiki ya matairi matatu maarufu kama bajaji na pikikpi ya matairi mawili maarifu kama bodaboda kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Babati kujitokeza kushiriki kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kuanza Novemba 27, 2024.


 Kaganda ametumia usafiri huo kuzunguka maeneo kadhaa ya Mji wa babati ikiwa ni pamoja na kwenye vituo vya wasafirishaji kwa njia ya pikipiki (bodaboda) na maeneo ya wajasiriamali wadogo kama mama lishe na wafanyabiashara wanaozunguka Mji huo.


Katika hotuba zake alizozifanya kwenye mikutano ya hadhara kwa kila kituo ametumia fursa hiyo kelimisha umma kuhusu uandikishaji wa daftari la mkazi na ule uandikishaji  wa kuboresha taarifa zao utakaowasaidia kufanya uchaguzi mkuu wa Mwakani.


"Ili mtu aweze kutumia haki yake kikatiba lazima apite katika mchakato huu ambapo wakazi wa kila eneo wanajiandikisha ili waweze kupata nafasi ya kupiga kura siku itakapofika siku ya tarehe 27, Novemba tumeona pia ni vizuri tukapita na timu hii ya maafisa usafirishaji kwaajili ya kutoa elimu na kuwakumbusha wananchi kwamba wanatakiwa kujiandikisha".


Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya ametumia fursa hiyo kujiandikisha katika daftari la mkazi katika mtaa wake kituo cha Mrara ambapo takribani Maafisa usafirishaji 09 ambao ni majirani zake nao wamejiandikisha pamoja nae.


Kufuatia zoezi hilo baadhi ya Maafisa usafirishaji wametoa pongezi zao kwa  Mkuu wa Wilaya kwa kuweza kushirikiana nao na kukiri baada ya kujiandikisha wataendelea kufanya hamasa kwa wenzao kwenye mitaa yao.

No comments: