Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akizungumza na wafanyabiashara wa Manyara |
Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda |
Na Epifania Magingo,Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe amewataka wafanyabiashara Mkoani Manyara kuwa na nembo zinazowatambulisha pamoja na kuzirasimisha katika mamlaka husika ili waweze kufanya Biashara zao ndani na nje ya nchi.
Amezungumza hayo wakati akifungua maonyesho ya wanyabiashara Tanzanate Manyara Trade Fear katika viwanja vya stendi ya zamani Wilayani Babati Mkoani Manyara
Kigahe amesema wafanyabiashara wanapaswa kubadilika Kifikra ili fursa zinazopatikana ziweze kuwa na mchango katika uchumi wao na kwamba fursa hizo zitumike vizuri katika kuzikuza na kuzitangaza.
"Fursa kusema ni raisi lakini kuzigeuza hizo fursa kuwa utajiri ni jambo lingine sasa hili tunatakiwa kuwa na mikakati ya pamoja ya kukuza, kutangaza lakini pia na sisi tunufaike na fursa hizo".
Aidha,Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema Mkoa wa Manyara unakua kiuchumi lakini pia una mazingira wezeshi katika kukua.
Kaganda amaeleza kuwa baadhi ya maeneo wameendelea kuongeza thamani ya mazao ndani ya Mkoa ikiwa ni pamoja na wachakataji wa maziwa, wachakataji wa ngozi na mambo mengine yanayofanana na hayo.
Kaganda amesema kuwa Mkoa wa Manyara unahitaji kuongeza nguvu ili kuendelea kuimarisha uchumi kwakuwa kuna vidogo zaidi ya 200 huku akiomba wawekesaji kujitokeza kwa wingi kuja kuwekeza na kubianisha kuwa Mkoa unamlighfu za kutosha.
"Ndani ya Mkoa wetu tuna viwanda zaidi ya 200 lakini vingi ni viwanda vidogo vidogo lakini bado tunahitaji wawekezaji wa viwanda vikubwa kwasababu maligafi tunazo lakini pia maeneo ya kuweza kuweka viwanda hivyo tunayo na tumetengeneza sheria ndogo ndogo ambazo pia zinawawezesha wawekezaji kuweza kufika na kuwekeza kwa uraisi zaidi".
Maonyesho ya tatu ya Manyara Trade Fear yameeandaliwa na Taasisi ya TCCIA ambapo kwa mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu isemayo "Manyara kwa Ustawi wa Biashara na Uwekezaji ".
No comments:
Post a Comment