Na: Mussa Juma,maipac
maipacarusha20@gmail.com
Timu ya Soka ya Majengo FC imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Chem chem CUP mwaka 2024 baada ya kucharaza timu ya bodaboda FC magoli 2-1.
Katika michezo huo wa fainali uliohudhuriwa na mamia ya watu, mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga .
Mkuu wa mkoa alikabidhi mabingwa hao kikombe na fedha taslimu kiasi cha sh 2.5 millioni, huku mshindi wa pili akipata zawadi ya sh 1.5 milioni na mshindi wa tatu Maklayoni FC akipata zawadi ya sh 1 milioni.
Kwa upande wa timu za Vijana chini ya miaka 18 Mkuu wa mkoa alikabidhi zawadi ya kikombe na fedha taslimu million Moja kwa mabingwa Maweni FC na mshindi wa pili alikuwa Kakoi FC aliyepata sh 600,000 huku mshikemshike FC akiwa wa tatu na kuzawadiwa Shilingi 400,000.
Kwa upande wa wasichana Upengo Queen ya Olasiti waliibuka mabingwa na kuzawadiwa shilingi 1.5 milioni na Mdori queen walikuwa wa pili wakizawadiwa million Moja.
Akizungumza baada ya kutoa zawadi, Mkuu wa mkoa Sendiga alisema serikali mkoa Manyara inaunga mkono michezo ambayo sasa inatumika kuhamasisha uhifadhi.
Alisema mashindano ya chem chem yamekuwa yakifanyika Kila mwaka na yamekuwa na hamasa kubwa hasa kwa vijana.
"Serikali tunapongeza chem chem kwa kuendelea kuandaa mashindano haya ambayo yanahamasisha Ulinzi wa Twiga na Uhifadhi wa mazingira"alisema
Alisema serikali mkoa Manyara pia inathamini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya chem chem na vijijini 10 ambavyo vinaunda Burunge WMA.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Babati Anna Mbogo alisema mashindano hayo yamesaidia sana kupunguza ujangili wilayani Babati na kuendeleza utalii.
Mbogo alisema Sasa vijana wengi wa Burunge WMA wamekuwa mabalozi wazuri wa utalii na Uhifadhi kwani manufaa wanayaona ya kutunza wanyamapori.
Mwenyekiti wa Burunge WMA, Erick lilayani alisema mashindano ya chem chem CUP yameimarisha uhifadhi na kukomesha ujangili katika eneo la Burunge.
Alisema Burunge WMA inapongeza Taasisi ya Chem chem kwa kuendelea kuendesha mashindano hayo na Kila mwaka yamekuwa. yakivutia watu wengi.
Jumla ya timu 35 zimeshiriki michuano ya Chem chem CUP mwaka 2024 kutoka vijiji 10 ambavyo vinaunda hifadhi ya jamii ya Burunge wilayani Babati mkoani Manyara.
Mwisho
No comments:
Post a Comment