Na: Epifania Magingo,Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Wafugaji Mkoani Manyara wameshauriwa kukata bima ili kujikinga na majanga yanapotokea ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa ,mafuriko,magonjwa au adha nyinginezo ambazo zinaweza kumsababishia hasara mfugaji.
Akizungumza katika wiki ya maonyesho ya Manyara Tanzanite Trade Feir Afisa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania(TIRA)kanda ya kati Gladys Steven amesema wafugaji wanapokuwa na Bima inawasadia kurudi katika hali yao ya kawaida wanapopata majanga.
Amesema,TIRA inaendelea kutoa elimu kwa wananchi wakiwemo wafugaji juu ya umuhimu wa kuwa na bima kupitia vyombo vya habari,maonesho, semina na mikutano.
"Bima ya kilimo na ufugaji zitamsaidia mkulima na mfugaji kujikinga na majanga yatakayotokea mfano unaweza ukategenea utalima kiasi Cha heka zako labda tano alafu utavuna kiasi Cha magunia 200 au 300 lakini ikitokea changamoto labda hali ya hewa au mafuriko basi utapa Kinga ya hiyo bima itakusaidia."
Nae,Afisa Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima Anna Massao, amewataka wananchi kutembelea banda la TIRA ili wajifunze mambo mbalimbali ikiwemo kazi kubwa inayofanywa na Mamlaka.
Amesema katika banda hilo wapo maafisa mbalimbali kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima(TIRA) ambao wanatoa elimu inayohusu bima lakini zaidi wanaelimisha fursa zilizopo katika Soko Kama kuwa wakala au washauri wa bima.
"Wananchi wajifunze kuhusu bima mbalimbali,bima za vyombo vya moto,bima za kilimo,wafugaji bima za nyumba na tunawaambia wananchi kwamba majanga hayana hodi".
Na,baadhi ya wafugaji ambao wametembelea banda la TIRA kwenye maonesho ya Manyara Tanzanite Trade Feir,wamesema awali walikuwa hawajui umuhimu kuwa na Bima hivyo elimu waliyopata imewapa ari ya kuamua kukata bima itakayowasaidia katika shughuli zao za ufugaji.
Wamesema elimu hiyo waliyoipata wataipeleka kwa wafugaji wengine ambao hawana uelewa huku wakiiomba Serikali kuendelea kutoa elimu mara kwa mara ili wapate miongozo namna ya kujiunga .
No comments:
Post a Comment