Na Epifania Magingo, Manyara
Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda ambae pia ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Wilaya amewahakikishia wananchi wote wa Wilaya ya Babati hali ya utulivu na amani katika upigaji wa Kura kwani wamejiandaa vyema na vikosi vya Jeshi la Polisi vitakuwa vikifanya kazi ya ulinzi na usalama kwanzia nyumbani wanapotoka wananchi hadi kwenye vituo vya kupigia kura.
Kaganda amesema maandalizi yote kwa ujumla yameshakamilika na mapema Novemba 27, 2024 wananchi wataanza kupiga kura kwaajili ya kuwapata viongozi wao wa Serikali za Mtaa.
Mkuu wa Wilaya Kaganda ameyasema hayo leo Novemba 26, 2024 wakati wa kukagua utimamu wa Vikosi vya Jeshi la Polisi vitakavyohusika na kusaidia zoezi la kulinda usalama siku ya hiyo kesho ya uchaguzi.
Wananchi wote wamehamasishwa kujitokeza kwa wingi ili kutimiza haki Yao ya msingi ya kupiga kura na kwamba wasiwe na hofu kwakua Ulinzi na Usalama uko imara.
Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali zà Mtaa hufanyika Kila baada ya Miaka 5 na kwamba ni Demokrasia ya Taifa la Tanzania.
No comments:
Post a Comment