Fountain Gate wajipanga vema kuikabili JKT Tanzania - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 24 November 2024

Fountain Gate wajipanga vema kuikabili JKT Tanzania

 


Kocha wa Klabu ya Fountain Gate Mohamed Muya akizungumza na waandishi wa habari za michezo



Na Epifania Magingo, Manyara 


Klabu ya Fountain Gate yenye makazi yake Wilayani Babati Mkoani Manyara iko katika maandalizi ya kujinoa kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na hivi karibuni inatarajia  kuchuana vikali na Klabu ya JKT Tanzania.


Akizungumza wakati wa mahojiaono na Wanahabari Kocha wa Klabu ya Fountain Gate Mohamed Muya  amesema Uongozi wa timu hiyo utajitahidi kufanyia maboresho kwenye timu ili kuifanya timu iwe bora na imara katika michuano yake unayofuata.


"Tutaboresha yale mazuri na kufanyia kazi mapungufu ili tuwe bora,tumejipanga madhaifu yaliyotokea katika mechi zilizopita yasijirudie ili tupate matokeo ya ushindi ili kurudisha faraja ya mashabiki,kwaio katika mazoezi tuko vizuri".


Wakati wakiendelea na  maandalizi hayo kwa Klabu ya Fountain Gate Msemaji wa timu hiyo Issa Mbuzi  amesema  michezo 11 imechezwa na kupoteza michezo mitatu na kwamba uongozi wa timu hiyo utasahihisha mapungufu yaliyojitokeza ili kufanya vizuri katika michezo inayofuta  dhidi ya timu za Yanga,JKT,Coast Union pamoja na Azam.


"Kwa sasa tunaendelea na maandalizi ya kupelekea mechi zetu nne ambazo zinakwenda kuhitimisha duru hii ya kwanza  ambapo amebainisha kwamba jana  imeongezeka timu nyingine ya CRDB Federation cup" Amesema Mbuzi.


Nao,baadhi ya wachezaji wa Klabu ya Fountain Gate wamesema maandalizi katika mechi zijazo yanaendelea kufanyika vizuri na kwamba mashabiki wakae kwenye mkao wa kupata matokeo mazuri kutoka kwa klabu hiyo.


"Upinzani ni mkubwa kwaio katika mechi zijazo nitajituma sana kuisaidia timu yangu iweze kufanya vizuri,na safari yangu  katika Klabu hii kuendelea kuitumikia kwa kiwango kikubwa ".amesema Selemani Mwalimu 


"Hakuna anayeenda uwanjani kupata matokeo mabaya,tuko katika mpango wetu ule ule wa kupambana ili mechi zetu za mbeleni turudishe moto wetu  tulioanza nao,sisi tunajiandaa pamoja na uongozi wetu unatuandaa vizuri ili tuweze kukabiliana na mpinzani wetu yoyote atakaekuja".amesema Salum Kiimbwa

No comments: