MBUNGE KOKA APIGA KURA, ASEMA UTULIVU NA AMANI CHANZO WANANCHI KUJITOKEZA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 27 November 2024

MBUNGE KOKA APIGA KURA, ASEMA UTULIVU NA AMANI CHANZO WANANCHI KUJITOKEZA








Na Julieth Mkireri, MAIPAC KIBAHA


MBUNGE wa Jimbo la Kibaha mjini Sylvestry Koka (CCM) ameshiriki kupiga kura katika kituo cha Mkoani A Uchaguzi Serikali za Mitaa.


Koka ambaye amefika kituoni hapo majira ya saa saba mchana baada ya kutembelea katika vituo vingine, ambapo amesema hali ya amani na utulivu imekuwa ni moja ya sababu wananchi wengi kujitokeza kupiga kura.


"Mwamko ni mkubwa wananchi wamejitokeza kupiga kura kutumia demokrasia yao ya kuchagua viongozi wanaowataka ," amesema


Mbunge huyo ameaema chama chake kinafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo jambo ambalo linampa mtumaini ya wagombea wa Chama hicho kuibuka na ushindi.


Awali mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge mapema saa mbili alikuwa kati ya wananchi waliowahi katika kituo hicho kupiga kura .


Kunenge amesema hali ya usalama imeimarishwa kwa wananchi wote watakaoenda kupiga kura kuchagua viongozi wao.


Charles Stephen na Frida Matata ni kati y wananchi waliojitokeza kupiga kura katika kituo cha Mkoani A ambao wamesema maandalizi ya vituo na vifaa vya kupigia kura yamerahisisha kuchukua muda mfupi wa kupiga kura.

Mwisho

No comments: