RC SENDIGA AWAHIMIZA WAUMINI KUJITOKEZA KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 1 November 2024

RC SENDIGA AWAHIMIZA WAUMINI KUJITOKEZA KUPIGA KURA SERIKALI ZA MITAA

 






Na Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga ambaye amemuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu kwa wananchi wa Mkoa huo kwamba Serikali ya awamu ya sita anayoiyongoza itaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi za Dini zote na Kanisa Katoliki Tanzania kuhakikisha Ustawi wa jamii na waumini wote unaimarika, umoja na mshikamano wa Serikali na Kanisa unaendelezwa.


Salamu hizo amezitoa wakati wa Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa la Roho Mtakatifu Parokia ya Babati yaani kuliweka Wakfu na kulitakasa kwaajili ya Maadhimisho Matakifu na pia waimarishwa Zaidi ya 200 wamepokea Sakramenti ya Kipaimara  yaani wamefanywa kuwa imara Askari hodari wa yesu Kristo, Misa ambayo imeongozwa na Mhasham Askofu Anton Lagwen wa Jimbo Katoliki la Mbulu.


Sendiga amesema, Rais Samia amemtuma kuja kuwakumbusha waumini wa Kanisa Katoliki kujitokeza kwa wingi November 27 kupiga kura ya kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji huku akiwaomba kwa nafasi zao kutoa hamasa kwa wengine kujitokeza kwakua ni haki Yao kikatiba.


"Ameushukuru Mkoa wa Manyara kwa kuandikisha Zaidi ya wanachi laki 8 sawa na asilimia 90, hivyo matarajio yake wanachi wote hao waliojiandikisha watakwenda kupiga kura na kuchagua Viongozi wao wa Serikali za Mitaa, vitongoji na vijiji". Alisema


Aidha, Sendiga ameahidi kuwa Uongozi wa Mkoa pamoja na Serikali kuu kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha na kuwa na upendo ili kuhakikisha Ustawi wa wananchi wa Manyara unimarika.


Awali,wakati wa Misa hiyo, Mhasham Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu Anton Lagwen amewaalika waamini wa  Kanisa hilo kujiombea na kuwaombea waimarishwa hao pamoja na familia zote kwa lengo la kupingana na adui wa roho ili kujiepusha kuingia katika matendo yasiofaa.


" Maadui wa roho ni wengi sana,ibilisi ni adui wa roho,tabia yangu mbaya ni adui wa roho,watu wabaya na wenyewe ni adui wa roho hasa wao wanakwamisha kwenye masuala ya Imani lakini pia mazingira yasiyoafaa ambayo unaweza ukajitumbikiza ni adui wa roho". Alisema 


Imeelezwa kuwa Kanisa la Roho Mtakatifu Parokia ya Babati ambalo limejengwa kwa miaka 11 huku Rais Samia alichangia ujenzi huo kwa kutoa Shilingi milion 100 na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ambapo Mgeni Rasmi katika Sherehe ya Kutabaruku Kanisa Hilo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga.


No comments: