Na Mwandishi wetu,Ruvuma
maipacarusha20@gmail.com
Wakili wa kujitegemea mkoa wa Ruvuma Dickson Nduguru ameitaka serikali kutunga sheria ngumu ambayo itawabana Viongozi au wadau wa habari wanaopiga waandishi wa Habari pindi wanapoenda kubalansi habari.
Ushauri huo aliutoa wakati akitoa mada ya uhuru wa kujieleza kwenye semina ya kijamii kuhusu kukuza uhuru wa kujieleza iliyofanyika mkoani Ruvuma ambapo Chama cha waandishi wa Habari mkoani humu kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za waandishi wa Habari nchini(UTPC) imeandaa mkutano huo.
Ndunguru alisema,uhuru wa kujieleza upo kisheria lakini unamipaka ili kuweza kuzuia chuki,machafuko,kuvunjiana heshima ,kuchafuana na hata kuoneana.
Akizungumza katika mkutano huo mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas aliwataka waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma kufanya kazi kwa kufata maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na kuwarudisha kwenye mstari waandishi ambao wanatoka nje ya mstari ili kuipa thamani na heshima taaluma ya uandishi.
Naye Sheikh wa mkoa wa Ruvuma Ramadhan Mwakilima alisema kila sehemu kuna taratibu zake hivyo haiwezekani kila mtu akawa anaeleza anachotaka lazima kuwe na mipaka.
Mwisho..
No comments:
Post a Comment