Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
WAKULIMA kutoka vijiji vinne vya kata ya Tomonto vikiwema lukonde na kungwe wilaya ya Morogoro wameiomba serikali kuweka nguvu ya pamoja katika kuendeleza matumizi ya mbegu za asili kwa wakulima hususani walioko vijijini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika maonyesho ya mazao na mbegu mbalimbali za asili yaliyofanyika katika kijiji cha kikundi, walisema mbengu za asili kama hazitaangaliwa na kupewa kipaumbele ziko mbioni kutoweka kabisa kitu ambacho si sahihi.
Zuhura Omary ni mmoja wa wakulima hao ambaye ameshiriki maonyesho hayo ya mbegu za asili, alisema mbegu za asili ni bora na zinatoa mavuno mengi ambayo yanafaa kwa biashara na chakula .
Aidha zuhura alisema kuwa chakula ambacho kimetokana na mbegu za asili kina kinga ya kutosha katika kupambana na magonjwa madogomadogo kwenye mwili wa binadamu, hivyo basi kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha wakulima wanatumia mbegu za asili ili kulinda afya za walaji.
Hata hivyo Zuhura alibainisha kuwa kilimo cha asili ni bora kutokana na mbegu hizo kuvumilia ukame, magonjwa na hakina gharama kubwa.
Hamis Semsagwe ni diwani wa kata Tomonto ambaye naye alieleza umuhimu wa mbegu za asili kwa wakulima na kusisitiza kuwa kila mkutano utakaofanyika ndani ya kata hiyo lazima utakuwa na agenda ya kuhamasisha matumizi ya mbegu za asili.
Kwa upande wake Afisa program jinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi kutoka PELUM Tanzania Anna Malwa alisema kuwa lengo la kufanya maonyesho hayo ya mbegu za asili ni kutokana na mbegu hizo kuonekana zinafanya vizuri zaidi.
Aidha alisema kuwa mbegu za asili pia zimeonyesha kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kuhifadhi chakula kwa muda mrefu.
Hata hivyo alisema vikundi hivyo vya wakulima ambavyo vinatumia kilimo ikolojia na wengi wao wakiwa ni wanawake vimeweza pia kutokomeza ukatili wa kijinsia katika familia kwa kutoa taarifa za ukatili kwa mamlaka husika.
Malwa alisema kuywa pamoja na kilimo ikolojia kinachofanywa na wanavikundi hao lakini pia wamekuwa wakisisitiza wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili waweze kuleta maendeleo na mabadiliko katika vijiji vyao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment