Na Epifania Magingo, Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amewataka wanufaika wa Mikopo ya Halmashauri ya Mji wa Babati kuzingatia na kufuata Mafunzo waliyopatiwa na Maafisa maendeleo ya Jamii kabla ya kupewa Mikopo hiyo.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi hundi za mikopo hiyo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati Kaganda amewataka wanufaika hao pale wanaopona kuna sitofahamu warudi kwa maafisa maendeleo ya jamii ili waweze kupata maelezo mazuri ya namna ya kuendesha shughuli zao ili kuweza kulipa mikopo hiyo kwa wakati.
Aidha,Kaganda amewataka wanufaika hao kutambua fedha walizozipata sio za hisani bali ni Mkopo unaotakiwa kurejeshwa kulingana na utaratibu uliowekwa ili na vikundi vingine viweze kunufaika na mikopo hiyo ya asilimia 10 ya Vijana, Wanawake na Makundi ya Wenye ulemavu.
"Mali bila daftari hupotea bila habari, tukazingatie sanaa mafunzo tuliyopewa ili yatusaidie kupiga hatua kutoka hapo tulipo kwenda hatua nyingine, hatutamani kuona wale mliochukua mikopo mnajificha na pale mtakapoona kwenye biashara yenu mnapitia magumu ni vizuri kurudi kwa Maendeleo ya Jamii ili wao watafute wataalamu wa kuja kukusaidieni".
Aidha ,Kaganda amewataka wanufaika wa mikopo kuendelea kuangalia fursa nyingine kama za kilimo kwani kilimo kwa Mkoa wa Manyara kinafanya vizuri ili kuweza kukwamua maisha ya kila mwannchi.
Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Babati Abdulrahman Kololi ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanufaika hao kuwa na matumizi mazuri ya fedha zao za vikundi ili kulinda amana ya vikundi vyao na kuweza kufanya marejesho kwa wakati, amewataka pia kufanya biashara zao wakijua kuwa ndizo zinazoleta mapato ya Halmashauri yanayosaidia kupata Mikopo hiyo wanayoipata.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA. Shaaban A. Mpendu amesema jumla ya shilingi Milioni 211 zilitengwa kwenye vikundi mbalimbali ikiwa ni mikopo ya Vijana, na wanawake huku akieleza kuwa kwa sasa hapakuwa na makundi maalumu aliyekuwepo alifariki kabla ya zoezi kukamilika huku akidaibkuwa shilingi milioni 211 tayari zipo kwenye vikundi ambavyo vimeundwa na kupata sifa.
Aidha, CPA Mpendu ameendelea kusisitiza kuwa katika Halmashauri yake kuna zaidi ya Shilingi Milioni 550 kwaajili ya kukopesha vijana, wanawake pamoja na makundi Maalumu, huku akitilia mkazo kuwa ni muendelezo wa jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakitari Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wao Wanufaika wa mikopo hiyo kupitia risala yao wamekiri kupokea mafunzo yatakayowasaidia kupata uelewa zaidi kwenye uendeshaji wa shughuli zao huku wakitaja kuwa Ofisi za maendeleo ya jamii zimekuwa zikiwapa ushirikiano kila wanapohitaji na watazidi kutumia ofisi hizo.
No comments:
Post a Comment