Na: Mwandishi Wetu
maipacarusha20@gmail.com
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) ametembelea maabara ya ithibati ya mazao ya nyuki inayosimamiwa na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kupitia Kituo chake cha Utafiti wa Wanyamapori Njiro ambacho kimejikita kwenye utafiti wa nyuki na mazao yake.
Mhe. Chana ametoa wito wa kukamilisha maabara hiyo ambayo itaongeza pato la taifa kwa kupata fedha za kigeni kupitia soko la kimataifa la mazao ya nyuki ikiwemo asali. Pia uchumi wa mtu moja kwa moja kwa wananchi.
“Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi Shupavu wa Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan inahakikisha wananchi wananufaika na fursa zilizopo kwenye maliasili ikiwemo sekta ya nyuki“ amesema Dkt. Chana
Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori Njiro Dkt. Wilfred Marealle amesema maabara hiyo inakamilishwa kupitia Mradi wa kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao ya nyuki (_*Beekeeping Value Chain Support Project - BEVAC_*) inatarajia kutoa huduma mwanzo mwa mwaka 2025 na itasaidia kuharakisha biashara ya mazao ya nyuki katika soko la kimataifa ambapo awali Serikali ilikuwa inatumia gharama kubwa kupeleka sampuli nje ya nchi kudhibitisha viwango vya ubora
“sample zilikuwa zinachukua muda mrefu kupata majibu na kusababisha kupoteza soko ” ameeleza Dkt. Marealle
Awali, Mhe. waziri amefanya kikao kwa njia ya mtandao na ujumbe kutoka idara ya Uvuvi na Wanyamapori ya Serikali ya Marekani ambapo kimehudhuriwa na wataalam ngazi ya Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Dkt. Alexander Lobora na watafiti wa TAWIRI wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Eblate Mjingo
No comments:
Post a Comment