DC NICKSON KUZINDUA KIBAHA SHOPPING MALL DEC 7 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 3 December 2024

DC NICKSON KUZINDUA KIBAHA SHOPPING MALL DEC 7





Na Julieth Mkireri, MAIPAC KIBAHA


maipacarusha20@gmail.com


MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson John anatarajia kuongoza wakazi wa mji wa Kibaha katika ufunguzi wa soko la maduka ya kisasa ya biashara (shopping Mall) lilipojengwa kwa gharama ya sh. Biln 8.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Dk Rogers Shemwelekwa ameeleza hayo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya hiyo ambapo amesema uzinduzi wa soko hilo utafanyika Desemba 7 mkabala na kituo cha mabasi


Dk.Shemwelekwa amewataka wananchi kujitokeza kushiriki uzinduzi wa soko hilo ambalo litakuwa na bidhaa mbalimbali za kisasa zikiwemo nguo ambazo mara nyingi wamekuwa wakizifuata jijini Dar es Salam.


"Wananchi sasa wamepata sehemu ya karibu ya kufanyia manunuzi Kuna maduka makubwa pale ndani yana nguo za kila aina nyingine hata Kariakoo huwezi kuzipata na bei zake ni rafiki kwa Jamii nawakaribisha kushiriki katika uzinduzi utakaofanywa na Mkuu wetu wa Wilaya kila mmoja aje ashuhudie mwenyewe," amesema.


Dk.Shemwelekwa ameishukuru Serikali kwa kuidhinisha fedha za ujenzi wa maduka hayo kwani kupitia soko hilo wakazi wa mji wa Kibaha watakwenda kuinuka kiuchumi.


Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya Nickson John amesema kikao hicho cha kamati ya Ushauri ni sehemu sahihi ya kupokea ushauri kutoka makundi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya hiyo.


Kadhalika amepongeza Mkurugenz wa mji huo kwa usimamizi wa mapato ambao umefanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo ikiwemo ununuzi wa madawati 4000 na sh. Milion 10 kwa kila kata kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara


Mwisho

No comments: