Pauline Gekulu Amshukuru Mungu kwa kumuepusha Tukio la Kumchafua Kisiasa - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 2 December 2024

Pauline Gekulu Amshukuru Mungu kwa kumuepusha Tukio la Kumchafua Kisiasa

 



Na Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Kufuatia tuhuma nzito za kufanyiwa vitendo vya ukatili kwa kijana anayefahamika kwa jina la Hashim Ally za kuingiziwa chupa za bia  njia ya haja kubwa, tuhuma ambazo  zilizokuwa zikimkabili kwa Muda mrefu Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Pauline Philipo Gekul kwa mara ya kwanza amezungumza na  kukanusha vikali kutohusika kitendo hicho. 


Mbunge Gekul amezungumza na waandishi wa Habari pamoja na wananchi wa Jimbo la Babati Mjini waliohudhuria hafla yake ya kutoa shukrani kwa Mungu iliyofanyika kwenye Hotel ya Paleii Lake View Garden Mkoani Manyara ambapo amesema tukio Hilo ni la kutengenezwa kutoka kuwa la kibiashara na kuwa la kisiasa kwa kutaka kumchafua.


Amesema na kudai kuwa,baada ya vipimo vya kitabibu  vilivofanyika kwa kijana Hashimu Ally cheti cha daktari kilithibitisha kuwa kijana huyo hakubainika kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji Kama ambavyo alivokuwa akijieza.


"Dakitari aliandika no any bruises, no injuries, hakuna jeraha lolote huko ambacho chupa zilitumika kuhifadhia, huko ndani hakupata jeraha,no injuries of the maana siwezi kutamka nadhani mmenielewa na baadae mtasoma waandishi.


"Mimi sikufanya ukatili, lakini nchi hii wenye kufanya makosa makubwa Jamhuri ndo inamshitaki mtu huyo aliefanya makosa na sio tu mtu wa kawaida, wale walioondoka kwenye kushitaki mahakamani, mahakama ilisikiliza na kuendelea na taratibu zake".


Awali, kabla ya hafla hiyo aliungana na waumini wa Kanisa la KKKT kutoa shukrani kwa Mungu kwa magumu aliyoyapitia huku akiongoza harambee ya uchangiaji wa fedha ili kumalizia ujenzi wa kanisa hilo ambapo  Shilingi milioni 116 zilipatikana huku fedha tasilimu zikiwa ni Shilingi milioni 90.


Nao, baadhi ya Viongozi wa Dini waliohuduria hafla hiyo wametoa msisitizo kwa wananchi kuona umuhimu wa kumtukia Mungu katika nyakati zote ngumu na za furaha na kutumia fursa hiyo pia kuwaombea Viongozi wa Serikali waweze kufanya kazi zao kwa uadilifu na uaminifu na kuzingatia maadili ya kazi,huku wakimtia moyo Mbunge huyo kuendelea kumuamini Mungu.


"Mitihani,majaribu hayo ni mambo ya kawaida katika maisha ,dhahabu lazima ipite kwenye moto lakini sisi tunaangalia dhahabu tu,na Hilo kushukuru mungu usiangalie kama uliumia wewe shukuru tu,sisi tunaangalia jinsi mungu alivokuasaidia" amesema mchungaji Jasson Kahembe


Mtihani uliomkuta akaona amlilie Mwenyezi Mungu muumba wa viumbe wote,na kwasababu limepita kwa kheri akaamua kufanya hivi,hii ndo ishara ambayo amefanya anamshukuru mungu juu yake kwa uwezo wake,na siku zote muegemee sana Mwenyezi Mungu kwa Kila kitu na iwe darasa kwa Kila mmoja".amesema Shekhe Hamis Ramadan

No comments: