Na Julieth Mkireri , Maipac KIBAHA
maipacarusha20@gmail.com
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri Wilaya ya Kibaha limepitisha makadirio ya bajeti ya sh. Bilion 39.6 kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Makadirio hayo ya bajeti yamepitishwa katika kikao maalumu cha Baraza hilo kilichokaa Januari 24 Mlandizi Wilaya ya Kibaha.
Akiwasilisha hoja katika kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Erasto Makala amesema kati ya fedha hizo sh. Bilion 30 ni kutoka Serikali kuu, sh. Biln 4.6 zitatokana na mapato ya ndani na sh. Biln 4 ni michango ya wafadhili.
Makala amesema ipo miradi mbalimbali itakayotekelezwa kupitia fedha za ndani ambayo ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya kuhifadhiwa maiti katika kituo cha afya Magindu ambayo imetengewa sh. Miln 50.
Miradi mingine ni ujenzi wa jengo la X- ray katika kituo cha afya Mlandizi uliotengwwa sh. Milion 100 na madawati 200 ambayo yataenda katika shule za Samia Mtongani (100) Boko Mnemela (50) na kawawa (50).
Amesema katika bajeti ya 2023/2024 Halmashauri ilipokea sh.Biln 32.8 sawa na asilimia 97 ya makisio ya mwaka ambayo ni sh. Biln 33.9.
Makala ameeleza kwamba hadi kufikia June 2024 Halmashauri hiyo imepata Mafanikio katika ujenzi wa shule mpya ya Sekondari sambamba na kuanzisha ujenzi wa soko la kisasa.
Katika Baraza hilo Madiwani wameomba Halmashauri kuangalia namna ya kukarabati barabara kwenye Mitaa yao pamoja na kuongeza idadi ya vyumba vya Madarasa kuwanusuru wanafunzi wasisongamane katika chumba kimoja.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Shukuru Lusanjala amesema bajeti hiyo ikipitishwa watasimamia utekelezaji wake kama ilivyopangwa kwa kuwagusa wananchi moja kwa moja.
Lusanjala pia wamesema kwenye maeneo yaliyoelezwa kuwa na barabara mbovu, uhitaji wa madawati na vyumba vya Madarasa watatafita namna ya kutatua kupunguza upungufu uliopo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment