SERIKALI KUENDELEA KUSAIDIA KAYA KWA TASAF - SIMBACHAWENE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 23 January 2025

SERIKALI KUENDELEA KUSAIDIA KAYA KWA TASAF - SIMBACHAWENE

 





Na Mwandishi wetu, Singida 


maipacarusha20@gmail.com 


WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa umma  na utawala bora George Simbachawene amesema Serikali itaendelea kuhakikisha kaya masikini zinajikwamua kiuchumi kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF unaotekelezwa  kwenye mikoa yote ya hapa nchini.


Waziri huyo  ametoa kauli hiyo mkoani Singida akiwa katika ziara ambapo amekutana na wanufaika wa mpango huo wa kunusuru kaya masikini kijiji cha Kinyakae manispaa ya Singida.


"Katika kipindi hiki serikali imeweza kuleta Bilioni 47.9 hapa singida zilizolenga kupelekwa kwa kaya masikini na miradi ambayo inagusa na kuondoa changamoto ndogondogo za wananchi ili waweze kufanya shuguhuli zao za maendeleo zinazolenga kuondoa umasikini, niwapongeze sana TASAF kwa hilo" alisema Waziri Simbachawene


"Jana nilikuwa nasikiliza ule mkutano mkuu wa CHADEMA nikamsikia Mbowe anasema kwa serikali ya CCM inataka kuondoa umasikini wa watu kwa TASAF kwa kuwagawia hela, nataka nimwambie Mbowe ndio serikali ya CCM inataka kuondoa umasikini wa watu wake wale wasiojiweza kabisa kwa kuwasaidia fedha"' Simbachawene


Amemaliza kwa kusema Serikali inatumia mfuko wa TASAF kuondoa changamoto zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja kwa kwenda kurekebisha miundombinu, vikwazo katika maisha yao.


Kabla ya kufanya ziara hiyo Waziri huyo amekutana na na baadhi ya viongozi na watumishi ofisi ya Mkuu wa mkoa ambapo ameonyesha kukerwa na uzembe unaofanywa na baadhi ya Maafisa Utumishi wa Umma hususani katika suala zima la upandishaji madaraja wafanyakazi pamoja na utatuzi  pwa migogoro.


MWISHO

No comments: