Mashabiki kuishuhudia Simba Mara ya Kwanza Mkoani Manyara - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 5 February 2025

Mashabiki kuishuhudia Simba Mara ya Kwanza Mkoani Manyara

 






Na Epifania Magingo, Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 



Mashabiki wa michezo Mkoani Manyara kwa mara ya kwanza Toka kuanzishwa kwa Mkoa huo wanashuhudia mtanange wa ligi kuu Tanzania NBC soka kati ya timu ya Simba  ambapo itawakutanisha na wenyeji Fountain gate fc.



Wakati huo huo Simba sc Klabu imewasili mkoani Manyara  tayari kwa mechi hiyo itakayochezwa tarehe 6 Februari mwaka huu kwa mara ya Kwanza tangu kuanzishwa kwa mkoa huo.


Kuelekea mchezo huo timu zote kupitia makocha na manahodha wa timu hizo wamezungumzia maandalizi yao huku klabu ya simba ikiwashukuru mashabiki wake kwa kuendelea kuwaunga mkono na kujitokeza popote timu hiyo inapokwenda kwaajili ya michezo yake.


Darian Wilken ambaye ni Kocha Msaidizi wa Klabu ya Simba amesema maandalizi ya kiufundi yako vizuri na kabla ya michuno hiyo timu hiyo itakua na mazoezi ya mwisho na kueleza kuwa wanafahanu wapinzani wao wa fountain wamejiandaa vizuri pia kwaio timu zote zinatarajia alama tatu muhimu.


Robert Matano ambaye ni Kocha Mkuu wa  Fountain Gate amesema aina ya mchezo ambao wanaenda kucheza unahitaji uangalizi mkubwa kwakua ni mchezo mgumu.

 

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa Tanzanite kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara.

No comments: