Na Epifania Magingo,Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ameongoza maadhimisho ya siku ya wanawake yenye lengo la kutoa fursa mbalimbali kwa Taifa hususani kwa wanawake ikiwemo kupima mafamikio yaliyofikiwa kimaendeleo, kuhamasisha usawa wa kijinsia na haki Kwa wanawake na kuimarisha hali ya kiuchumi kisiasa na kijamii.
Maadhimisho hayo kwa Mkoa wa Manyara yamefanyika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika viwanja vya Hydom ambapo kitaifa siku ya wanawake Duniani yatafanyika 8 machi 2025 uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Akizungumza na wanawake waliohudhuria maadhimisho hayo 5 machi 2025 Sendiga ameeleza kuwa katika Mkoa wa Manyara inaonyesha kuwa kundi la Wanawake na wasichana, limekua likiathirika kutokana na vitendo vya ukatili wa Kijinsia, kutokupewa haki ya kupata elimu kwa watoto wa kike, kunyimwa haki ya kumiliki ardhi au mali katika familia, usawa katika mgawanyo wa madaraka, na kukosa uhuru wa kuwa sehemu ya maamuzi.
"Tunaishukuru Serikali na wadau mbalimbali kwa Jitihada mbalimbali zilifanyika kuondoa vitendo vya ukatili na kuleta usawa wa kijinsia, kwa kuwa kuwajengea uwezo watoto na Wanawake pamoja na makundi mbalimbali katika jamii kubaini viashiria vya ukatili na kutolea taarifa, na utoaji wa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu ili kuweka mazingira rafiki ya makundi yote kupata huduma bora na kujikwamua kiuchumi" Amesema RC Sendiga.
Sambamba na hilo RC Sendiga, amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Wajasiriamali katika viwanja hivyo pamoja na kutoa vyeti vya pongezi, tuzo, hati za ardhi kwa Wanawake ambapo pia Mkuu wa Mkoa Queen Sendiga amepata tuzo ya mwanamke kinara kwa Mkoa wa Manyara.
Akihitimisha hutoba yake RC Sendiga, amewapongeza Wanawake wa mkoa wa Manyara kwa kufanya shughuli mbalimbali katika wiki hii ya maadhimisho (tarehe 1 hadi 4) kama kutembelea watu/watoto wenye mahitaji maalumu , wagonjwa,wafungwa na kutoa elimu ya usawa wa kijinsia na ulinzi wa mtoto kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Siku ya wanawake Duniani kwa mwaka 2025 imebabwa na kauli mbiu isemayo,"Wanawake na wasichana 2025, tuimarishe haki, usawa na Uwekezaji ".
No comments:
Post a Comment