Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
CHAMA cha Wafanyakazi wa Reli Tanzania (TRAWU) kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada za kuendelea kuboresha mashirika ya TRC na TAZARA, pamoja na kwamba bado kumekuwepo na changamoto ya kutosainiwa kwa mkataba wa Hali bora kwa wafanyakazi wa TRC ambapo kimemuomba Rais kuingilia kati suala hilo.
Akizungumza mkoani Morogoro kwa niaba ya wajumbe wa baraza kuu la Trawu taifa baada ya kumalizika kwa vikao vya baraza hilo katibu mkuu wa Trawu Taifa Juma Masoud alieleza kuwa wamelazimika kufanya hivyo kutokana na masuala mbalimbali ya wafanyakazi wa TRC na TAZARA kutofanyiwa utekelezaji na menejimenti.
Masoud alisema kwa upande wa shirika la reli Tanzania na Zambia serikali imefanikiwa kulipa mishahara kwa wafanyakazi, kuendelea kuboresha miundombiu ya reli kila inapo hitajika pamoja na serikali kuendelea na mchakato wa kupata mwekezaji wa kuboresha na kuendeleza TAZARA ili kuleta ufanisi na tija.
Aidha alisema kwa upande wa TRC, Serikali imefanya ukarabati wa njia ya reli ya zamani y MGR kwa kubadilisha reli ya zamani iliyokuwa na uwezo mdogo wa kubeba mizigo na kuweka reli mpya za ratili 80 kuanzia Dar es salaam hadi Isaka huku kazi nyingine ikiendelea upande wa Tabora hadi Mpnda.
Akizungumzia suala la mishahara Masoud alipongeza namna serikali ilivyopandisha mishahara kwa wafanyakazi wa TRC na ulipaji wa madeni sugu ya wafanyakazi, kupanda kwa madaraja wafanyakazi ambayo yalikwama kwa muda mrefu, kufufuliwa kwa safari ya treni ya Dar es salaamu kwenda mikoa ya Kilimanjaro na Arusha pamoja na ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa.
“Watanzania ni mashahidi kwa kazi iliyofanywa na serikali hii ya awamu ya sita juu ya ujenzi wa miundombinu ya reli,ununuzi wa treni za EMU pamoja na kuanza kwa safari ya treni ya umeme kutoka Dar es salaa na Dodoma, ujenzi wa SGR umeongeza ajira kwa watanzania na kupunguza ugumu wa maisha na tunamshukuru Rais Samia kwa kwa kuendelea kutoa ajira kwa sekta ya reli hasa vijana,”alisema.
Katibu mkuu huyo akasema,pamoja na jitihada hizo za serikali katika kuboresha shirika la reli, changamoto ya kubwa inayowakabili ni wafanyakazi wa Tazara ni suala la Mishahara kwamba kwa mwezi Februari 2025 wafanyakazi hao hawajalipwa huku chama Trawu kikiamini kuwa kuwepo kwa uzembe unaofanywa na menejimenti ya TAZARA kwa kutokusanya madeni kwa wawekezaji wanaotumia reli hiyo “OPEN ACCES FEE”.
Kwa upande wake mwenyekiti wa TRAWU taifa Jacob Shindika alisema chama kimekuwa kikipitia changamoto mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa majukumu yake kama kuzuiliwa kufanya shughuli za kisheria ndani ya TRC jambo linalowanyima wafanyakazi haki yao ya kukutana na chama chao na kueleza matatizo waliyonayo kwa viongozi wa chama.
“Chama kimekuwa kikiandaa barua mbalimbali kuomba kufanya majukumu yake bila mafanikio na badala yake kutishwa na kubadhalilishwa kwa viongozi bila kujua tatizo au kuna kitu gani kinafichwa ili chama kisifahamu,”Kuna tete kuwa kuanzishwa kwa chama kingine chenye nia ya kuilinda menejimenti jambo linalofanya ugumu wa Trawu kufanyakazi kwa uhuru na kisheria,”alisema Shindika.
Naye mwenyekiti wa kamati ya wanawake TRAWU Froida Mwakatundu alieleza kuwa kwa sasa wafanyakazi wa TRC wanafanyakazi wakiwa na mawazo ya kufikiria kustaafu kwao kwani wakimaliza muda wa utumishi wao kazini hulipwa sh milioni 1 hata kama mtumishi huyo atakuwa ametumikia shirika hilo zaidi ya miaka 40 kwa mujibu wa “Scheme Incentive” iliyopo.
Alisema suala la Mkataba wa Hali bora kwa wafanyakazi wa TRC, rasimu ya mkataba huo ilishapatikana na upo hatua za mwisho ili usainiwe ila menejimenti ya TRC imekataa kumalizia kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Chama hicho cha Trawu kikatoa Ombi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuingilia kati changamoto hizo ambazo zinalenga kuichonganisha Serikali na wananchi na kwamba chama kinaamini Rais ni msikivu, mwenye kuchukua hatua kupitia falsafa ya 4R.
No comments:
Post a Comment