FUSO LAGONGANA NA LORI LA MAFUTA MOROGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 25 April 2025

FUSO LAGONGANA NA LORI LA MAFUTA MOROGORO

 




Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


Ajali ya gari mbili,Fuso iliyokuwa imebeba  Kokoa lililokuwa likitokea Ifakara wilayani Kilombero  kugongana na Lori lenye Tanki la Mafuta lililokuwa likitokea Jijini Dar es salaam kuelekea Tunduma Mkoani Songwe na kusababisha majeruhi moja kondakta wa Fuso ambaye dereva wa gari Hilo alikimbia baada ya ajali.


Afisa wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Morogoro,Inspekta Fadhil Makalla alisema ajali hiyo imetokea saa 10 jioni, Aprili 25,2025 na kusababisha majeruhi huyo moja ambaye jina lake Bado halijafajamika aliyepelekwa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Kwa matibabu zaidi.


Alisema walipata taarifa kutoka jeshi la Polisi na walipogika walimkuta majeruhi huyo moja ambaye ni kondakta wa Fuso aliyekuwa amenasa mguu wake wa kushutona kufanikiwa kumtoa na kumoeleka hospitali.


Inspekta Makalla alisema ajali ilitokea eneo la Kasanga kata ya Mindu ambapo gari aina ya Fuso lililobeba Kokoa ambayo Bado haijachakatwa ilikuwa ikizipita Bajaji mbili nipo alipokutana na Lori la Mafuta na kugongana.


"Katika harakati ya kukwepana ziligongana Kila moja kwenda kugonga mti, ambapo Fuso ilipochanika na mzigo wa magunia yaliyobeba Kokoa kipasuka na kumwagika barabarani na kusababisha foleni hii kubwa mnayoiana,"alisema.


 Alisema Hali ni shwari na Zimamoto na Uokoaji imewasiliana na wakala wa barabara Tanzania Tanroads mkoa wa Morogoro ili iweze kuja na boza la maji Kwa ajili ya kusafisha barabara.


Mashuhuda wa ajali hiyo Omary Hassan alisema chanzo Cha ajali alivyoshuhidoa ni dereva wa gari ya Fuso alipokuwa akitaka kuzipita Bajaji.


Nae shuhuda Aman Mustafa aliomba Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na mamlaka nyingine kushirikiana kuondoa Kokoa zilizoanguka ambazo zinasababisha kuteleza kwa gari,Bajaji na pikipiki ambazo zinaweza kusababisha ajali nyingine hasa kipindi hiki cha mvua


Mwisho..

No comments: