NACTVET YABAINI VYUO VYA AFYA VILIVYOFUNGIWA NA KUENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA KOZI ZILIZOFUTWA KISHERIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 16 April 2025

NACTVET YABAINI VYUO VYA AFYA VILIVYOFUNGIWA NA KUENDELEA KUTOA MAFUNZO KWA KOZI ZILIZOFUTWA KISHERIA

 






Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi(NACTEV) limebaini uwepo wa  Chuo feki Cha afya kinachodaiwa kuwa na matawi yake katika mikoa ya Njombe, Morogoro na Dar es Salaam kikitoa fomu na kusajili wanafunzi na kufundisha kozi ambazo zilishafutwa kisheria.


Aidha Chuo hicho Cha afya Cha Highlands kilishafungwa lakini kimegunduliwa kinatumia majengo ya Chuo kingine Cha afya Cha St Malkus ambacho nacho kimefungwa na kipo kwenye uangalizi na Nactvet.


Meneja wa Mitihani na Utunuku kutoka Nactvet Dk Obeid Mahenya alisema hayo mkoani Morogoro wakati timu ya maafisa ukaguzi ya Nactvet iliyofika katika chuo cha Afya cha St Malkus (St Malkus College of Health and Allied Sciences(SMCOHAS) ambacho kilishafungiwa kutokana na kutokidhi vigezo vya ubora.


Dk Mahenya akatahadhalisha wazazi,walezi na wanafunzi wanaosoma ama wanaotarajia kujiunga na kozi mbalimbali za afya kujiadhali na vyuo vinavyotoa mafunzo ya afya ambavyo avijasajiliwa kwani baadhi vinafanya udanganyifu.


Alisema chuo hicho pamoja na kufungiwa kimekuwa kikitumia njia nyingine ya udanganyifu kwa kutumia jina la chuo cha afya cha Highland kampasi ya Morogoro (Highlands Health Institute Morogoro Campus), hivyo njia hiyo imekuwa ikiwafanya kuendesha mafunzo ya afya ambayo hayatambuliki.


“Kinachoendelea hapa ni utapeli mtupu, tumekuja kufuatilia taarifa ambazo tulizopata kutoka kwa wadau wetu kwamba kuna chuo kinaendesha mafunzo ya afya lakini hakija sajiliwa na tumekuja kujilidhisha, lakini kwa bahati mbaya ama nzuri tumekuta jina linalotumika na chuo chenyewe ni tofauti ambacho kabla ya hapo tuliwahi kukifungia,wamebuni jina lingine na wanatumia njia kuwadanganya wananchi na kuendesha mafunzo yasiyotambulika, ”alisema Dk Mahenya.


Alisema wamefanya ukaguzi kwenye maeneo mbalimbali na kukagua na kuona ratiba na mitihani lakini baada ya kuzungumza na mkuu wa chuo hicho ambaye pi ni mmiliki kwa njia ya simu alidai kuwa yeye haendeshi mafunzo na hawezi kufanya hicho kitu na kinachoonekana ni utapeli.


Akawataka watanzania, walezi na wazazi kujihadhali na vyuo kama hivyo vya utapeli vinavyotoa mafunzo na kuwaomba kutumia tovuti ya Nactvet ama website ambayo inaonyesha vyuo vyote vilivyosajiliwa ambavyo vimeruhusiwa kutoa mafunzo.


Aidha Dk Mahenya alisema kwa taratibu za Nactvet, hatua ya kwanza ya kuchukua kwa chuo hicho kuutarifu Umma, hatua ya pili ni kuandika taarifa na kukiandikia barua rasmi na kuendelea kukifatilia ikionekana anaendelea watafikishwa vyombo vya kisheria,pamoja na kukifungia mara ya kwanza alifuata taratibu ya kufanya maombi na ulipofanyika ukaguzi ilionekana bado hajakidhi viwango vya kutoa mafunzo na kupewa muda wa kuboresha maeneo na vifaa vya kujifunzia, na kufundishia ili aje akaguliwe tena.


“Lakini hapa katikati kabla ajakaguliwa tena amehamua kukiuka kanuni na kuanza kutoa mafunzo jap kaja kwa jina lingine, kwa sheria ni kwamba anahatarisha uwezo wa kupata usajili unazidi kuwa mgumu na mwisho wa siku itabidi tumpeleke kwenye vyombo vya sheria,”alisema.


Naye mthibiti ubora mwandamizi wa Nactvet Florian Everest alisema katika ukaguzi huo wamegundua chuo kipo chini ya uangalizi wa baraza kwa maana kuwa kilipewa muda wa kuboresha mazingira yake na udhahifu uliyokutwa ili baadae kiweze kukaguliwa na baadae kuruhusiwa kufundishwa lakini cha kushangaza kimekutwa kinatoa program ambazo kwa sasa hazitambuliki kwa soko la ajira.


Everest alitaja program ambazo hazitambuliwi kwa sasa kuwa ni Medical Labaratory, Health Assistant na Clinical Medicine na kwamba hiyo imeweza kuwafikirisha sana.


Alisema uraghai unaofanywa na wamiliki wa vyuo hivyo kwa njia ya udanganyifu wengi wao wanafahamu na kuelewa kabisa umuhimu wa usajili wa vyuo, kwani chuo kinaposajiliwa baraza linakuwa linatoa muongozo, linasimamia mafunzo kwa kukagua mazingira ya ufundishaji kwa maana ya ubora , sifa za wanachuo wanaojiunga, walimu wanaofundisha na kuangalia mazingira ya chuo kama yanafaa kwa kuendesha mafunzo hayo na kabla ya yote baraza linajiridhisha kama mtaala unaofundishwa ni ule wenye mahitaji sokoni.


“Kama wangekuwa wamefuata taratibu hizo zote chuo wasingeanzisha progaramu ya health Assistant kwa sababu hiyo ilishafuntwa na kwa soko la sasa la afya waajiri hawahitaji tena watu wenye ujuzi wanaotokana na program hiyo,”alisema.


Mmiliki wa chuo hicho Luqman aliyejitambulisha kwa jina moja .…. alipozungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu alisema wao kwa sasa wapo vizuri na wanafunzi wanaotoka katika chuo cha Highlands wanapata ajira na kwamba wanatambulika na Nactvet na kwamba mwezi wa tano nactvet wakifungua dirisha na kuanza kusajiliwa,wao kama chuo wataanza kuchukua wanafunzi mwezi wa kumi ndio watawaingiza.


“Kama hawa wa kozi ya Health Assistant kwa sababu hawapitii hilo dirisha hawa tumeshaanza kuwachukua kuna inteki ya mwezi wa tatu tunaruhusiwa kuwachukua na kusajili majina kwa hiyo tunaendelea kupokea na mwezi huu wan ne, lakini kwa hawa wa Clinical Medicine hata wanaosajiliwa mwezi wa tano wanasubiri mpka mwezi wa kumi,”alisema.


.......

No comments: