Mratibu wa
UKIMWI wa Halmashauri ya Mji Kibaha Siwema Cheru akifundisha maafisa elimu kata katika semina ya VVU na Ukimwi mjini Kibaha |
NA: JULIETH MKRERI, MAIPAC KIBAHA
HALMASHAURI ya Mji Kibaha imeendesha semina ya kuwajengea uwezo maafisa Elimu
kata,walimu wa shule za Msingi na Sekondari kuhusiana na masuala ya
VVU/UKIMWI mahala pa kazi kwa lengo la kuondoa unyanyapaa na ukatili wa
kijinsia.
Mratibu wa
UKIMWI wa Halmashauri ya Mji Kibaha Siwema Cheru amesema semina hiyo ni
mwendelezo wa Mafunzo mengine ambayo yamekuwa yakitolewa kwa wadau
mbalimbali ili kuondoa vitendo vya unyanyasaji sehemu za kazi na kwamba
sasa wamefikiwa waratibu wa Elimu kata na walimu ambao ni wadau wakubwa
kwenye jamii na wanakaa na wanafunzi muda mrefu.
Baadhi ya Walimu wakiwa katika semina ya VVU na Ukimwi |
Mwezeshaji
katika semina hiyo Dk.Mariam Ngaja ameeleza kuwa kupitia semina hiyo
witawajenge uelewa walimuwa na watakuwa na wanawajibu wa kuwafundisha
wanafunzi wao kuhusu afya ya uzazi kwa Vijana na maradhi
yanayoambukizwa kwa njia ya ngono na Elimu ya dawa ya kulevya.
Ngaja
ameongeza kuwa semina hiyo ambayo ni ni ya kawaida na ni utekelezaji wa
mkakati wa nne wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI Tanzania hasa kwa wasichana
balehe, Vijana na wanawake.
Mmoja
wa walimu Augustine Seso ameishukuru Halmashauri kwa kuwapatia semina
hiyo na kwamba imewafikia muda muafaka na sasa wanakwenda kwenye jamii
kutimiza lengo la kutoe Elimu ili kuondosha unyanyasaji na ukatili wa
kijinsia kwenye jamii.
Picha ya pamoja mara baada ya kupata mafunzo kwa maafisa elimu hao |
No comments:
Post a Comment