NEMC WAJIVUNIA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA,WASEMA ALIKUWA INJINI YA MAFANIKIO TANGU AKIWA MAKAMU WA RAIS - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 4 March 2023

NEMC WAJIVUNIA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA,WASEMA ALIKUWA INJINI YA MAFANIKIO TANGU AKIWA MAKAMU WA RAIS

Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Tarifa la hifadhi na Usimamizi wa mazingira(NEMC) Dkt.Samweli Gwamaka akizungumza na Wandishi wa Habari juu ya utekelezaji wake

 


Na Shakila Nyerere,Dodoma

maipacarusha20@gmail.com

 Mkurugenzi mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira[NEMC]Dkt. Samwel Gwamaka amesema, wanajivunia mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita ambayo Kwa kiasi kikubwa yalichochewa na Dkt.Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa sasa wakati ule akiwa Makamu wa Rais.


"Tunamshukuru na kumpongeza sana Mhe. Rais Samia,kwani mafanikio mengi ambayo tumeyapata ndani ya miaka hii miwili ,yeye alikuwa mhimilli mkubwa katika kuanzisha na kusimamia michakato mingi ya mabadiliko ikiwemo katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki,hivi leo Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazojivunia kukomesha matumizi ya mifuko ya plastiki -hii yote ni jitihada za Rais Samia wakati ule akiwa Makamu wa Rais "amesema Dkt.Gwamaka.



Aidha ameyataja mafanikio mengine waliyoyapata ndani ya miaka hii miwili kuwa ni pamoja na kuanzisha sera mpya ya mazingira ya mwaka 2021 huku akisema kuwa sera iliyokuwepo ambayo ilitungwa mwaka 1997 pamoja na uzuri wake lakini ilikuwa haiendani na Muda, mazingira na kasi ya maendeleo na madiliko ya sayansi na Teknolojia,tumeboresha upatikanaji wa huduma zetu kwa wateja wetu ambapo sasa huduma ni masaa 24, Kuongezeka Kwa ofisi za Kanda Kutoka 5-13,Uteuzi wa wakaguzi wa mazingira 405,Kuongezeka Kwa mapato yaliyowezesha NEMC kuchangia kiasi Cha shilingi bilioni 9 Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita,Upandaji wa miti maeneo mbali mbali ya nchi,utoaji wa vibali n.k


"Pamoja na mafanikio hayo,bado tunazo changamoto kadhaa na katika kukabiliana nazo ,tunayo Mipango mbali mbali katika kukabiliana nazo ikiwemo ya kuwekeza katika kutoa elimu ya mazingira na uhifadhi wa mazingira Kwa wananchi,Uanzishaji wa klabu za mazingira mashuleni[ Shule za msingi na sekondari] na Mipango mingine mingi."amesema DK.Gwamaka


Tunatoa rai Kwa wananchi kutuunga mkono katika mipango na Utii wa sheria na kanuni mbali mbali za uhifadhi,utunzaji na ustawishaji wa mazingira.Hatutasita kuchukua hatua kali za kisheria Kwa yeyote atakayekiuka sheria,taratibu na kanuni zilizowekwa.


No comments: