GODBLESS LEMA AMUOMBA RAIS SAMIA MADINI YA TANZANITE YAUZWE ARUSHA MJINI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 4 March 2023

GODBLESS LEMA AMUOMBA RAIS SAMIA MADINI YA TANZANITE YAUZWE ARUSHA MJINI

GODBLESS LEMA akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo 

 




Mwandishi wetu, Maipac

maipacarusha20@gmail.com


Mwenyekiti  Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema amemuomba , Rais  Dk Samia Suluhu Hassan kuondoa Marufuku ya kuruhusu Tanzanite kuuzwa Arusha na miji mingine kwani Kuzuia ni Ujima.

Lema amesema  hayo katika Mkutano wake na vyombo vya Habari Jijini Arusha Leo Machi 4,2023  na kueleza  Kuuzwa Madini ya Tanzanite Katika Mjii wa Mererani Pekee ni   kosa la Kimkakati na la Kibiashara.

Amesema kuwa  ni wakati Sasa Serikali  Kuruhusu Mfumo wa Biashara  Huria kwa Madini  ya Tanzanite Ili yapatikane kwa wepesi Ndani na nje ya Nchi .

Lema Ameitaka kudhibiti madini kutoroshwa serikali inatakiwa kuwa na utaratibu wa kutoa certificate maalum ya kuonesha madini halali.

Lema Amebainisha Kuwa Mfumo wa Soko Huria katika Uuzaji wa Madini ya Tanzanite Utaongeza Mapato ya Serikali na hivyo kuchangia Ukuaji wa Uchumi wa Nchi ya Tanzania.


Amesema kuwa  Arusha Ni Jiji la kitalii hvyo Serikali inapaswa Kuruhusu Biashara hyo Kufanyika Arusha mjini kupitia Broka ambao Wana leseni za Kufanya Biashara hyo Ili kuwezeshaji upatikanaji wake kwa wepesi.

Amesema walioleta hoja ya Kuzuia biashara ya Tanzanite kufanyika nje ya Mererani wanamawazo ya ujima kwani duniani ya Sasa jambo hilo haliwezekani.

"Leo ulienda nchi za Afrika ya Kusini,Kenya Dubai utakuta Tanzanite lakini Arusha hakuna Tanzanite"amesema

No comments: