JULIETH MKIRERI , MAIPAC KIBAHA
maipacarusha20@gmail.comMKUU
wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametembelea katika kongani ya viwanda
ya Sino Tan iliyopo Kwala wilaya ya Kibaha kukagua maendeleo ya ujenzi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Kunenge amesema amefanya ziara hiyo kuona
maendeleo ya mradi huo ambao ni wa uwekezaji mkubwa wa viwanda zaidi ya
300 katika mkoa huo.
Amesema
kiwanda cha kwanza katika Kongani hiyo kitaanza kufanya kazi Juni na
ajira 5000 zitatolewa na mradi ukikamilika ajira 100,000 kwa awamu ya
kwanza zitapatikana.
"Ahadi
yangu eneo hili litakuwa kubwa kwenye uwekezaji na wanaoanzisha Kongani
watakuja kujifunza hapa mpangiliio na kila kitu" amesema.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa amesema baada ya kikao hicho na kufanya mkutano wa
pamoja na wataalamu kutoka kwenye Taasisi watakuwa na utaratibu wa
kukutana mara kwa mara kutatua vikwazo vinavyojiyokeza kwenye mradi huo
ili uweze kukamilika kwa wakati.
"
Tumekubaliana hizi taasisi zinazohusika na kuunganisha huduma kwenye
hii kongani zikutane na uongozi wa SINO TAN ili waonyeshwe ramani hii
itasaidia kutoharibu miundombinu na kupunguza gharama za ziada" amesema
Kunenge.
Kwa mujibu wa
Kunenge Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)
wanatarajia kutatua kikwazo cha maji mwezi huu huku mahitaji ya umeme wa
Megawat 50 yakiwa yanashugjulikiwa na Tanesco na kufikia Juni tatizo
katika huduma hizo litakuwa limeisha.
Mwenyekiti
wa Kongani hiyo Janson Huang amesema ifikapo June mwaka huu kituo cha
huduma kitakuwa kimekamilika na kiwanda cha kwanza kitaanza kazi.
Katika
ziara hiyo Kunenge ameambatana na Watendaji kutoka katika ofisi yake na
Taasisi wezeshi zitakazohusika kufikisha huduma katika eneo hilo
wakiwemo TANESCO, TARURA, RUWASA na DAWASA .
No comments:
Post a Comment