BALTON TANZANIA WAZINDUA MBEGU BORA ZINAZOKABILIANA NA UKAME - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 8 March 2023

BALTON TANZANIA WAZINDUA MBEGU BORA ZINAZOKABILIANA NA UKAME

 



Mkurugenzi wa Balton Tanzania Chris Keeping akizungumza na wakulima pamoja na wasambazaji wa mbegu nchini katika uzinduzi wa shamba darasa  kwa wakulima nchini



Mgeni Rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania(TASTA) Bob Shuma akizungumza na swakulima na wasambazaji wa mbegu katika uzinduzi wa shamba darasa hilo

Meneja Mkuu wa Balton Tanzania Ravi Periyasamy akizungumza na wanahabari katika shamba darasa



Mmoja wa wataalamu wa shamba akilelezea manufaa aliyoyapata katika uzinduzi huo


Wakulima wakipewa elimu ya  nyanya zinazovumilia hali ya ukame




NA: ANDREA NGOBOLE,.Arusha

maipacarusha20@gmail.com

Kampuni ya usambazaji wa mbegu ya Balton Tanzania,imezindua mbegu mpya ambazo zinaweza kukabiliana na Ukame nchi ili kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali na hivyo kuuza mazao nje ya nchi.


Akizungumza katika uzinduzi wa mbegu hizo na mafunzo ya Shamba darasa kwa wakulima , Mkurugenzi Mtendaji wafanyabiashara wa Mbegu Tanzania(TASTA) Bob Shuma, amesema mbegu bora ndio Suluhu ya kuongeza Uzalishaji wa chakula.

Shuma amewataka wakulima kujifunza matumizi ya mbegu bora ili kuongeza uzalishaji wa mazao.yao.

Amesema, mbegu bora ambazo zinazalishwa na taasisi ya Balton Tanzania na taasisi nyingine zikitumiwa vizuri, Tanzania itakuwa na uwezo wa kuongeza uzalishaji wa chakula na hata kuuza nje na hivyo kuongeza mapato ya kigeni.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Balton Tanzania na Rwanda, Chris Keeping amesema kama wakulima nchini Tanzania, wakipata mbegu bora wanaweza kuongeza uzalishaji wa chakula na hivyo kuuza nje mazao yao.


Keeping amesema mbegu ambazo wameanza kuzisambani za za nyanya, vitunguu,pilipili hoho,., kabeji , tikiti maji na mboga mboga ili wakulima wazitumie mbegu hizo kuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali na kuweza kuuza mazao nje ya nchi"alisema


 Meneja wa Balton Tanzania, Ravi Periyasamy amesema taasisi hiyo, itaendelea kutoa mafunzo kwa wakulima na wasambazaji mbegu nchini,ili kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.


Periyasamy mbegu mpya ambazo zimeanza kusambazwa na taasisi hiyo, zinazingatia athari za mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yamesababisha kupungua kwa uzalishaji wa chakula.


Mkulima Meshack lwenje amesema uzalishaji wa mazao Yao imeshuka kutokana na kupungua mvua na kukosa mbegu ambazo zinastahimili Ukame.


Mfanyabiashara wa mbegu Delinetha John wa duka la Fide Mamba la Babati mkoa Manyara alipongeza Balton kwa kuja na mbegu bora ambazo zinastahimili Ukame.


No comments: