WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA KASI YA UPIMAJI ARDHI TANGA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 8 March 2023

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA KASI YA UPIMAJI ARDHI TANGA

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na wananchi waliohudhuria kikao alichokiitisha wilayani Handeni, mkoani Tanga ili kukabidhi rasmi mradi wa makazi maalum katika kijiji cha Msomera kwa Wilaya za Handeni na Kilindi.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda akizungumza na viongozi na wananchi waliohudhuria kikao cha kukabidhi rasmi mradi wa makazi maalum katika kijiji cha Msomera kwa Wilaya za Handeni na Kilindi kilichofanyika wilayani Handeni

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda akizungumza na viongozi na wananchi waliohudhuria kikao cha kukabidhi rasmi mradi wa makazi maalum katika kijiji cha Msomera kwa Wilaya za Handeni na Kilindi kilichofanyika wilayani Handeni



 

Baadhi ya viongozi na wananchi waliohudhuria kikao cha kukabidhi rasmi mradi wa makazi maalum katika kijiji cha Msomera kwa Wilaya za Handeni na Kilindi kilichofanyika wilayani Handeni.

 

Na. Hassan Mabuye, Tanga

 

 maipacarusha20@gmail.com


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka maafisa ardhi na maafisa mipango miji katika halmashauri zote nchini kuongeza kasi ya upimaji ardhi na kutoa hati kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ili kuepuka ujenzi wa makazi holela.

 

Ametoa kauli hiyo Machi 7, 2023 wakati akizungumza na viongozi na wananchi waliohudhuria kikao cha siku moja alichokiitisha wilayani Handeni, mkoani Tanga ili kukabidhi rasmi mradi wa makazi maalum katika kijiji cha Msomera kwa Wilaya za Handeni na Kilindi.

 

"kila mwananchi wa wilaya hii na nchi nzima anayemiliki ardhi lazima eneo lake lipimwe na apatiwe hati, Wizara ya Ardhi pamoja na TAMISEMI zimeisha agiza kwa maafisa mipango miji na maafisa ardhi kuchagua maeneo ya kupanga, kupima ili kutangaza viwanja na kutoa hati kwa wananchi" amesema

 

Aidha, amesisitiza miji yote nchini lazima ingizwe kwenye ramani za mipango miji ili kila mmoja ajulikane yupo wapi hasa ikizingatiwa kwa sasa tuna anuani za makazi na kuingizwa katika mfumo wa kielektroniki.

 

Naye, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda ameitaka ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Tanga na halmashauri zake kuongeza kasi ya upimaji ardhi katika maeneo mbalimbali ili kuepuka uvamizi wa maeneo ya watu na maeneo ya hifadhi.

 

"Kamishna wa Ardhi mkoa wa Tanga jitahidi usimamie upimaji wa ardhi wa mkoa huu mkoa usingekuwa na matatizo yoyote ya ardhi kama tungepima haya maeneo, sehemu kubwa kwasababu tuna zembea mpaka wananchi wanaenda wanavamia halafu ndio tunataka sasa kuwaondoa kwa vurugu" alisema Mhe. Pinda.



Katika kutilia mkazo suala hilo Mhe. Pinda aliwashauri viongozi wa Halmashauri kuepuka kuingia kwenye maeneo ambayo yamekatazwa kabla kuingia kwenye mazungumzo kuhusu umiliki wa eneo husika kwa sababu inawachanganya kwenye maamuzi.

 

Kijiji cha Msomera kilichopo wilayani Handeni kwa sasa ni makazi ya wananchi ambao kuanzia Juni, 2022 walihama kwa hiyari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro ili kulinda ikolojia na uoto wa asili katika eneo hilo. Mara baada ya kuwasili, walipewa nyumba za kuishi za ukubwa wa vyumba vitatu kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 2.5 na  jingine la malisho la ekari tano

No comments: