TPHA WABORESHA MFUMO WA UCHAMBUZI WA VIUATILIFU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 1 March 2023

TPHA WABORESHA MFUMO WA UCHAMBUZI WA VIUATILIFU

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea DK.Joseph Ndunguru akizungumza na Waandishi wa Habari Jijin Dodoma juu ya utekelezaji wa Majukumu yake

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea DK.Joseph Ndunguru akizungumza na Wandishi wa Habari Jijin Dodoma juu ya utekelezaji wa Majukumu yake

 

Na Shakila Nyerere, Maipac Dodoma

maipacarusha20@gmail.com

Mamlaka ya Afya ya Mimea na viwatilifu (TPHA)imepima afya za watumiaji wa viuatilifu 403 kwenye mashamba ya maua ambapo watumiaji 70 sawa na 17.36% walipatikana na athari zinazosababishwa na utumiaji wa viwatilifu.


Akizungumza na Wandishi wa Habari Leo march 1,2023 Jijin Dodoma Kaimua Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea DK.Joseph Ndunguru amesema katika Mwaka wa fedha 2022/2023 katika utekelezaji wa Majukumu ni pamoja na kupima Afya za watumaiji wa viwatilifu ili kuwa na watu wenye kujua Afya zao zipoje.


Hata hivyo amesema Mamlaka imeboresha maabara za kikemia na kibaiolojia na imefanikiwa kupata ithibati kwenye maabara ya uchambuzi wa viuatilifu (ISO 17025:2017)pamoja na Kuboresha mfumo wa utoaji huduma ambao ni mfumo rafiki kwa wadau, unawapunguzia wateja gharama za ziada, na  unatoa vibali kwa haraka,  na unaonesha taarifa za ukusanyaji wa mapato ya Mamlaka.


Aidha amesema Mamlaka imefanya uchambuzi wa sampuli 1,025 za viuatilifu ambapo sampuli 1,005 sawa na 98.04% zilikidhi viwango na sampuli 20 sawa na 1.96 %

Kwakushirikiana na Wizara ya kilimo, imefanya uchambuzi wa sampuli za udongo takribani 1,300 kutoka kwenye mashamba ya “Block farming”. Ili kuwezesha biashara ya mazao, sampuli 40 zilifanyiwa uchambuzi kwenye mazao mbalimbali na sampuli zote zilikidhi viwango na biashara ya mazao ilifanyika. 


Katika hatua nyingine Mamlaka imeweza kudhibiti mlipuko wa Panya katika Mikoa mbalimbali ambapo jumla ya eneo la ekari 122,190 liliokolewa na uvamizi wa panya.uthibiti wa nzi ambapo jumla ya lita 585 za kiuatilifu aina ya Methyl Eugenol zimesambazwa katika wilaya mbalimbali nchini kwa ajili ya kudhibiti nzi wa matunda ilikuongeza tija na ubora wa matunda.


Huku akitaja uthibiti wa ndege aina ya kwelea kwelea milioni 227.4 na kufanikiwa kuokoa Tani 1056.3 za mazao ya nafaka. Aidha, kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la kudhibiti nzige wekundu (IRLCO-CSA), Mamlaka imefanya ufuatiliaji kwa njia ya anga kwenye mazalia ya asili ya nzige wekundu kwenye jumla ya hekta 195,150 kwa kutumia helikopta na kubaini hekta 1,000 zilizokuwa na kiwango kikubwa cha nzige.


"Mamlaka inategemea kuanzisha maabara ndogo kwenye vituo 17 vya ukaguzi Mipakani, inaendelea kuimarisha Maabara ya “Tissue culture” kwa ajili ya mimea pia itaendelea kuwajengea uwezo wataalamu wa Mamlaka katika kusimamia na kudhibiti milipuko ya visumbufu kwa wakati.Kutumia “DNA technology” katika kutambua aina za wadudu na magonjwa ya mazao ili kuwa na udhibiti endelevu na kuweka mfumo wa ufuatiliaji wa viashiria  vya uwepo wa mlipuko wa visumbufu.

Kuendelea kufanya ukaguzi wa viuatilifu wa mara kwa mara kwa watengenezaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji  ili kupunguza athari ya kuwepo kwa viuatilifu bandia. Katika kipindi hiki, mamlaka inafanya ukaguzi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya, Njombe, Iringa, Songwe, Morogoro na Mbeya.Kufanya utafiti kwenye vinasaba ili kukidhi ubora wa mbegu zenye kuhimili magonjwa na visumbufu na kufanikisha upatikanaji wa ithibati katika maabara za afya ya mimea (ISO 17020: 2012).Kuendelea kuimarisha majaribio na usajili wa wadudu marafiki na kuimarisha uchunguzi wa kimaabara kwa ajili ya visumbufu vya mimea hapa nchini."amesema DK Ndunguru 

No comments: