Baadhi ya wakina Mama WA KKKT Jimbo la Arusha wakiwa katika semina |
Na Onesmo Elia Mbise -Arusha
Katika Kuelekea Kilele Cha Maadhimisho Ya Siku Ya wanawake Duniani, Idara ya wanawake katika Kanisa La kilutheri Tanzania Jimbo La Arusha mashariki Dayosisi Ya Kaskazini Kati Wamekemea Ukatili Kwa Wanawake Pamoja Na Unyanyasaji w Kijinsia Unaendelea katika Mkoa wa Arusha na Maeneo Mengine ya Nchi ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Wanawake Jimbo La Arusha Mashariki Nembris Samweli ameeleza kuwa Dunia Ya Sasa Imejaa Ukatili wa Kijinsia Haswa Kwa Wanawake na watoto wadogo na katika Hili wanawake Wote Duniani wanapaswa kuungana na kuelimisha Jamii Ili Kuondokana Na Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia.
"Tunapoelekea Katika Kilele Cha Maadhimisho ya wanawake Duniani sisi wanawake Tunapaswa kuungana pamoja na kupinga Ukatili Wa kijinsia Kwa watoto wa kike kwani Kina Mama Ndio walezi wa Familia Zetu"
Nembris Amesema kuwa Wanawake ndio walezi wa Familia kuanzia ngazi ya kulea watoto Kiakili, na kueleza Jamii jinsi ambapo Familia nyingi zinapitia matatizo Kwa Kuwaona Ndgu zao wakifanyiwa Ukatili, na Hata Ubakaji.
Naye Narivi Peta Kyamba Amesema kuwa Mwanamke akisimama katika Jamii atalisimamisha Taifa kiuchumi, kijamii na Hata katika Nyanja za Kiungozi hvyo Wanawake wanaweza kuleta Mabadiliko katika Kutokomeza Ukatili na Unyanyasaji kwenye Jamii.
Amesema Kuwa Mwanaumke Anaweza kusimamisha Uchumi wa Nchi kwani wanawake ndio nguzo katika Familia na kwamba katika Dunia Ya Sasa wameongeza Nguvu katika Kujimarisha kiuchumi.
Ukatili na Unyanyasaji wa Kijinsia tayari inaonekana Kuwa ni Changamoto Kwa Jamii za mikoa Ya Kaskazini na Tanzania Kwa Ujumla.
No comments:
Post a Comment