WCF YAONGEZA KIMA CHA CHINI CHA FIDIA KUFIKIA 275,333 KWA MFANYAKAZI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 2 March 2023

WCF YAONGEZA KIMA CHA CHINI CHA FIDIA KUFIKIA 275,333 KWA MFANYAKAZI


Mkurugenzi wa Mfuko wa FIDIA Kwa wafanyakazi(WCF) John Mduma akizungumza na Wandishi wa Habari hiii Leo March 2/2023 Jijin Dodoma wakati akiwaeleza utekelezaji wa Majukumu yake ya Mwaka wa Fedha 2022/2023

Wandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mfuko wa FIDIA Kwa wafanyakazi WCF alipokua akiwaeleza Majukumu ya mfuko huo katika utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Picha zote na Shakila Nyerere



Na: Shakila Nyerere , Maipac Dodoma

maipacarusha20@gmail.com

Serikali kupitia WCF imetekeleza Sera ya kuongeza kima cha chini cha fidia hadi kufikia Shilingi 275,333 kutoka utaratibu wa awali ambao haukuwa na kima cha chini cha fidia kwa mfanyakazi ambaye hakupata ulemavu wa asilimia 100 


Hayo yamesemwa Leo March 2/2023 na Mkurugenzi  wa Mfuko wa Fidia Kwa wafanyakazi(WCF),  DKT. JOHN MDUMA wakati akizungumza na Wandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Tasisi hiyo Kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.


DK.Mduma amesema kupitia Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya maboresho kadha wa kadha katika kutelekeza andiko maraafu kwa jina la Blueprint ambaponi pamoja na kuweka usawa kwa sekta zote yaani Sekta za Umma na binafsi


Amesema Serikali imepunguza kiwango cha kodi ya malimbikizo ya madeni ya michango ya nyuma wanayo daiwa waajiri kutoka asilimia kumi (10%) hadi asilimia mbili (2%) ili kuhamasisha waajiri ambao hawajajisajili waweze kujisajili na watekeleze wajibu wao wa kulipa michango kwa ajili ya kulinda wafanyakazi wao dhidi ya majanga yatokanayo na kazi


Hata hivyo amesema  Serikali kupitia WCF imetekeleza Sera ya Msamaha wa Riba kwa waajiri waliochelewesha michango tangu Mfuko ulipoanza mwaka 2015 hadi Juni 2022 kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na kuondoa mzigo kwa waajiri ambao hawakuweza kulipia wafanyakazi wao kwa sababu mbalimbali ,Uamuzi wa kushusha viwango vya uchangiaji kwa Sekta binafsi unalenga kumpunguzia mzigo mwajiri ili fedha alizokuwa akitumia kuchangia zielekezwe kwenye maeneo mengine ya uendeshaji wa shughuli zake za uzalishaji

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mfuko wa FIDIA Kwa wafanyakazi WCF alipokua akiwaeleza Majukumu ya mfuko huo katika utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Picha zote na Shakila Nyerere



Kusajili Waajiri Tanzania Bara, hadi kufikia tarehe 30 June 2022, WCF imesajili jumla ya waajiri 27,786 ikiwa ni asilimia 90 ya waajiri 30,846 walioko kwenye kanzidata ya Mfuko na kufikia Mwezi Februari 2023, WCF imesajili jumla ya waajiri 29,978 pia kutoka Machi 2021 hadi Februari 2023 WCF ilisajili jumla ya waajiri 5,250


Amesema Waajiri wakubwa wanachangia kiasi kinachozidi Shilingi Milioni 1.5 kwa mwezi, waajiri wa kati wanaochangia kati ya Shilingi 250,000 na Shilingi Milioni 1.5 kwa mwezi na waajiri wadogo

wanachangia chini ya Shilingi 250,000 kwa mwezi


Na kusema Mfuko ulianza rasmi kukusanya michango kwa Waajiri kuanzia tarehe 1 Julai 2015. Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2022, makusanyo ya jumla ya michango yalifikia Shilingi Bilioni 545.49


"Shilingi Bilioni 88.07 zilikusanywa mwaka wa fedha 2020/2021 na Shilingi Bilioni 86.65 zilikusanywa mwaka wa fedha 2021/2022

Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2022, Mfuko umekusanya jumla ya Shilingi Bilioni 241.48 toka kwenye mapato yatokanayo na uwekezaji

WCF ilitengeneza Shilingi Bilioni 69.86 katika mwaka wa fedha 2020/2021; na Shilingi Bilioni 74.29 katika mwaka wa fedha 2021/2022

Jumla ya mali za Mfuko hadi 30 Juni 2022 ni Shilingi Bilioni 545.16 "amesema DK. Mduma


Hata hivyo amesema Kulipa Fidia Stahiki kwa wakati kwa wafanyakazi wanaopata majanga yatokanayo na kazi, mwaka 2021/2022 pekee, WCF ililipa fidia kwa wanufaika takribani 1,600 kwa zaidi ya Shilingi bilioni 9.33.Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2022, WCF imelipa mafao yenye thamani ya Shilingi Bilioni 44.61 kwa wanufaika mbalimbali


Amesema Katika kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2022,  WCF ililipa mafao ya jumla ya Shilingi Bilioni 6.19 kwa wanufaika 1,004 na hivyo kufanya wanufaika wa Mfuko toka kuanzishwa kwake kufikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya Shilingi Bilioni 49.44 na kukamilIsha kutumika muongozo wa kubaini magonjwa yanayosababishwa na kazi pamoja na mwongozo wa kutathmini magonjwa na ajali


"WCF inajukumu la kutoa Elimu kwa Umma kupitia semina, mikutano, maonesho na vyombo vya habari ikiwa ni pamoja na magazeti, redio, luninga, mitandao ya kijamii na vipeperushi  inatoa huduma kupitia mtandaoni kwenye usajili wa wanachama, kutoa vyeti vya usajili, kuwasilisha michango ya kila mwezi, kuwasilisha taarifa za ajali, ugonjwa au kifo cha mfanyakazi kilichotokana na kazi na kufuatilia mwenendo wa madai" amesema DK. Ndumba


Na kusema Hadi kufikia tarehe 30 Juni 2022, WCF imetoa mafunzo kwa madaktari 1,401 nchini ili kuwezesha kufanyika tathmini za magonjwa yatokanayo na kazi kwa ufanisi


Mfuko umekuwa ukilipa fidia kwa mfumo wa pensheni ya kila mwezi kwa wategemezi au wafanyakazi waliopata ulemavu unaozidi asilimia 30 inayofikia hadi asilimia 70 ya mshahara ikiwa wa ni pamoja na Kutekeleza Matakwa ya Katiba na Mikataba ya Kimataifa Kuongeza Tija katika Uzalishaji kupitia kuwapa fursa waajiri kujikita katika uzalishaji na kupunguza migogoro ya kazi


Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ni taasisi ya hifadhi ya jamii kwa lengo la kulipa fidia kwa wafanyakazi wanaopata ulemavu au kufariki kutokana na magonjwa au ajali zitokanazo na kazi wanazozifanya kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira



No comments: