MIAKA 39 TANGU KUFARIKI SOKOINE BADO AKUMBUKWA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 15 April 2023

MIAKA 39 TANGU KUFARIKI SOKOINE BADO AKUMBUKWA


Mtoto WA kwanza Edward SOKOINE, Joseph SOKOINE akiwa na Mama zake KATIKA Misa Maalum ya kukumbuka kifo Cha SOKOINE KATIKA Kanisa la Katoliki parokia ya Emaereti kigango Cha Enguiki    


Mwandishi wetu, Monduli 

maipacarusha20@gmail.com


Watanzania wametakiwa  kumuenzi hayati Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine kwa  kupiga vita ufisadi ,Rushwa,uhujumu uchumi kwa vitendo.


Hayati Edward Moringe April 12, 2024 ametimiza miaka 39 tangu kufariki kwa ajali ilivyotokea Mkoani Morogoro mwaka 1984 .


Wakizungumza katika kumbukumbu hiyo eneo la Monduli juu, juzi viongozi wa dini, serikali na kisiasa walieleza ni muhimu viongozi wote kumuenzi Sokoine kwani alikuwa mzalendo,alipiga vita rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Taifa, Fadhili Maganya  alisema taifa litaendelea kumuenzi Sokoine kwa uadilifu wale,uchapakazi,uzalendo na kuchukuwa rushwa na ufisadi.


"CCM tutaendelea kumuenzi  mchango wa Sokoine katika kupiga vita rushwa , ufisadi kwani alikuwa ni kiongozi mwadilifu"alisema


Alisema Sokoine licha ya kufariki miaka 39 lakini ameacha alama katika taifa na anaendelea kuenzia jambo ambalo tunapaswa kuiga.


Askofu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki(KEKAM) ,Philemon Mollel Lengasi alisema Rais Samia Suluhu ameonesha kuchukizwa na ufisadi hivyo anapaswa kuwawajibisha wote waliotajwa na CAG katika ufisadi.


"Mama achukuwe hatua wote waliotajwa kuhusika na ufisadi , amezungumza kwa uchungu na sisi kama viongozi wa dini tunamuunga mkono"alisema


Alisema  katika kumuezi Sokoine viongozi waliohusika na ufisadi wachukuliwe hatua.



Mwenyekiti wa CCM Mkoa Arusha, Zelothe Stephine alisema katika kumuezi Sokoine viongozi wanapaswa kuwa waadilifu kwani Sokoine ameacha alama.


"Sokoine alikuwa mchapakazi, mwadilifu,mwaminifu,mchamungu na alipenda Taifa lake"alisema


 Fred Lowassa ataka heshma ya Sokoine kulindwa.


Mbunge wa Jimbo la Monduli, Fred Lowassa alisema heshma aliyoacha Sokoine Monduli pamoja Edward Lowassa ni lazima ilindwe .


"Hawa wazee wameacha heshma kubwa katika Jimbo la Monduli , Sokoine atakumbukwa kwa kisimamia vita dhidi ya rushwa na Lowassa kupambana na suala la elimu"alisema


Alisema heshma ya wilaya ya Monduli iliyojengwa na Sokoine na Lowassa inawalazimisha kila kukicha viongozi kujiongeza katika Utendaji kazi.


Mkuu wa wilaya ya Monduli,Joshua Nassari alisema kuna mengi ya kujifunza kupitia Sokoine kwani amecha historia ambayo haiweze kufutika.


Akizungumza kero za wilaya hiyo,Nassari alisema hatawaangusha viongozi waasisi wa wilaya hiyo na atafanyakazi kutatua kero za Wananchi Monduli.


Paroko la Kanisa la Katoliki parokia ya Emaereti kigango Cha Enguiki Anodi Baijukie alisema viongozi wanapaswa kuongoza kwa kuacha alama nzuri 


"Kiongozi ukifanya mambo mazuri utakumbukwa kama ambavyo Sokoine Leo tunamkumbuka"alisema.


Mtoto wa Sokoine,Balozi Joseph Sekoine aliwashukuru Watanzania kuendelea kumuezi Sokoine.


Amesema familia yao Inashukuru Watanzania wengi  na Serikali hadi sasa kuendelea kusimamia mambo ambayo aliyaamini Sokoine ikiwepo vita dhidi ya uhujumu uchumi.


Alisema mwakani familia yao itaaanza maadhimisho makubwa ya kitaifa ya kumbukumbu ya miaka 40 tangu kufariki Sokoine.






No comments: