NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC KIBAHA
HALMASHAURI
ya Mji Kibaha kupitia Zahanati ya Mwendapole iliyopo Kata ya Kibaha
imeratibu jopo la Wakunga wabobezi wanaotarajia kutoa Elimu kwa
wajawazito Aprili 6, 2023 ili kunusuru afya ya Mama na Mtoto wakati na
baada ya kujifungua.
Hayo
yameelezwa mjini Kibaha na Prisca Nyambo msimamizi wa huduma za uzazi
Kibaha ambaye pia ni Mkunga ambaye alitaja huduma zitakazotolewa kuwa
ni uchunguzi wa kina na maendeleo ya ujauzito Maandalizi ya Kujifungua,
Uchunguzi wa dalili za hatari kwa mjamzito, lishe bora,upimaji wa
vipimo mbalimbali pamoja na kutoa ushauri.
Nyambo
amesema Zahanati ya Mwendapole imekuwa na wateja wengi wa kujifungua
kutokana na huduma bora zinazotolewa kwani takwimu zinaonyesha kuwa kati
ya wajawazito 140 hadi 180 hupokewa kwa Mwezi kuanza huduma za Kliniki.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mshamu Munde amesema nia ya Serikali ni
kupunguza ama Kuondoka kabisa vifo kwa wajawazito na watoto ambapo
alitoa rai kwa Wakunga wote kuwa karibu na wajawazito na wawe na kanzi
data maalum itakayowasaidia kuwafuatilia.
Naye
Diwani wa Kibaha Goodluck Manyama ameishukuru Serikali kupitia
Halmashauri ya Mji Kibaha kwa kufanya utaratibu huo ambao unakwenda
kutoa uhakika wa afya za Watoto watakaozaliwa
Halmashauri
ya Mji Kibaha yenye hospitali,Vituo vya afya na Zahanati 25 zinazotoa
huduma ya Mama na Mtoto,kwa Mwezi hupokea kati ya akina mama 600 hadi
650 wanaofika kujifungua.
Inmeelezwa
kuwa utaratibu kama huo ni kwa mara ya kwanza kufanyika katika zahanati
hiyo na unatarajiwa kufika katika maeneo mengine ya Kongowe,Msangani na
Viziwaziwa.
No comments:
Post a Comment