ADA TADEA WAIPONGEZA SERIKALI KUSITISHA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YA HALMASHAURI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 20 April 2023

ADA TADEA WAIPONGEZA SERIKALI KUSITISHA MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YA HALMASHAURI





Mwandishi wetu, Maipac  Arusha 


maipacarusha20@gmail.com


Chama Cha Ada Tadea kimepongeza hatua ya serikali kusitisha mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake na vijana nchini ambayo ilikuwa inatolewa na halmashauri na kueleza mikopo hiyo ilikuwa inatawaliwa na mizengwe, rushwa na ukiukwaji wa taratibu.


Katibu Mwenezi Taifa Chama cha Ada Tadea, Zuberi Mwinyi

Akizungumza na Maipac Media Tanzania Jana amesema mikopo hiyo ilikuwa na sintofahamu nyingi sana ikiwemo wengi wao waliokuwa wakipewa ni makada wa chama cha mapinduzi.na ndugu wa watendaji wa Halmashauri. "


"Sisi Ada Tadea tunamuunga mkono Rais Samia Suluhu  tunaamini safari yetu ya  demokrasia ya kweli ndio imeanza sababu haki zikifanyika kwa wote hata mungu atajaalia nchi yetu na atatuepusha na mabalaa yanayoandama dunia ikiwemo ushoga na usagaji"amesema 


Mwinyi amesema mikopo ilikuwa ni kwa wanaCCM pekee,  kama mtu sio CCM kupata mkopo ilikuwa ngumu sana hivyo tunaamini mambo mengi yatakuwa mazuri, hata ile inayosemekana kuwa kuna vikundi hewa  vingi si vingi kama vinavyosemwa hapo ilikuwa  Makada na ndugu wa wafanyakazi wa Halmashauri.


Mwinyi amesema suala la kupelekwa hela zote kwenye mabenk hiyo ndio itakuwa suluhisho la jambo hilo hata wale wapigaji sasa watakuwa wamedhibitiwa na upatikanaji wake hautakuwa na uchama tena.


Fedha nyingi pia zimepotea kwa sababu kuna vikundi vilikopeshwa baada ya hapo kukaingia covid, vita vya ukreni na ukame hilo pia limechangia wengi kushindwa kufanya marejesho hivyo hilo pia serikali iliangalie kwa kina, watu wamepitia vipindi vigumu sana. 


Amesema vitendo cha kuhamishia fedha hizo benk inamaana hata usalama wake utakuwa mkubwa sababu zitakatiwa bima hata kukitokea madiliko ya mazingira au hali ya hewa bima italipa hasara hiyo sio kama zilipokuwa hazina ulinzi wowote. 


Pia tunashauri serikali iwaangalie na wafanyabiashara wadogo wadogo ili nao waweze kupatiwa mikopo hiyo ya asilimia 10% kutoka kwenye halmashauri zao sababu kundi lingine ni kundi la wafanya biashara si wote wanamiradi sababu lengo kubwa ni kuwaendeleza wananchi. 


Mwinyi ameshauri bunge hilo  litengeneze  sheria kali kwa watakao husika kula fedha za miradi ili kila mtu aogope, na sio mpaka kutokee tatizo ndio swala linazungumziwa, tunakuwa watu wa matukio, ni lazima viongozi wawe wabunifu  kwaajili ya masilahi ya nchi yetu, sababu hivi sasa kuna mfumuko wa bei inabidi serikali iweke kipaombele  kitu kama hiki kuona watapunguzaje ukali wa maisha kwa wananchi wake. 


"Kwa ushauri wangu haya yote yanayotokea hivi sasa utatuzi wake ni  yaweze kutengenezewa sheria kali  ili pindi mchakato wa katiba mpya utakapoanza iweke  sheria kali ya kuwabana  wasio wazalendo wanaokula fedha za miradi ya wavuja jasho"amesema 


No comments: