Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza wakati WA uzinduzi wa daraja |
NA JULIETH MKIRERI, MAIPAC MKURANGA
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge Aprili 26, 2023 amezindua Daraja la Mipeko iliyopo Barabara ya Mwanambaya lililojengwa kwa gharama ya sh Milion 214.
Akizungumza na Wananchi wa Mipeko Kunenge amepongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta Maendeleo ambayo yanawagusa wanachi wa kawaida.
Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa Rais Samia alipofanya ziara Mkoani Pwani alieleza nia yake ya kuhakisha Mkoa huo unapata miundombinu yote Muhimu ya Afya, Elimu, Maji, Nishati, Barabara.
Ameshikuru kwa namna ambavyo utekelezaji unaendelea na kwamba Mkoa huo una Mtandao wa Barabara wa km 6629 zinazohudumiwa na TANROADS na TARURA.
Amesema Bajeti ya kutekeleza shughuli za Barabara kwa mwaka 2021/22 ilikuwa ni Bilion75.5 na kwa mwaka 2022/23 imeongezwa kufikia Bilion 81.
Ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mkuranga kupanga Mji wa Mkuranga kwa kuwa Mji huo unakuwa kwa kasi na kwamba Serikali inafanyia kazi maombi ya Wananchi hao ya kujengewa Kituo cha Afya, kupelekewa Umeme na ujenzi wa Daraja.
No comments:
Post a Comment