Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis akijibu swali Bungeni |
Na WMJJWM, DODOMA
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mwanaidi Ali Khamis ametaja sababu kubwa za Watoto kuishi na kufanya kazi katika mazingira hatarishi ni malezi duni, migogoro ya Kifamilia, Makundi rika, umaskini wa kipato ndani ya familia na unyanyasaji majumbani.
Naibu Waziri ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma leo Aprili 20, 2023, wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa viti maalum Mhe.Tamima Haji Abasi juu ya tafiti na jitihada zilizofanywa na Serikali kutatua Changamoto ya Watoto wa Mitaani.
“Serikali inaendelea na mkakati wa kutoa mafunzo ya Malezi kwa Watoto katika ngazi ya Familia, jitihada ya kuwakutanisha watoto hao na Wazazi wao lakini pia kuwahudumia watoto wasio na Wazazi katika vituo vya kulelea watoto hao”amesema Mhe.Mwanaidi
Mhe. Mwanaidi ameongezea kwamba, Serikali itaendelea kufanya tafiti katika mikoa yenye changamoto zaidi ya kuwa na Watoto wengi wa Mtaani.
“Nitoe Rai kwa wazazi na Walezi kuhakikisha watoto wanapata Malezi Bora,kuthamini watoto wote kwani Mtoto ni Taifa la kesho” amesisitiza Mhe.Mwanaidi.
No comments:
Post a Comment