Baadhi ya wananchi na askari wakiotoa miili ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo
Na Mwandishi wetu
maipacarusha20@gmail.com
Watu wanne wa familia moja wamefariki dunia na wengine wawili wameokolewa baada ya gari waliokuwa wamepanda kusombwa na mafuriko ya maji katika eneo la Kin’gori kata ya Malula Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha mapema leo
Akizunguma na wanahabari KATIKA eneo la tukio mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh Emanuela Kaganda amesema kuwa gari iliyosombwa na maji ni aina ya Noah yenye Namba za usajili T 499 DMY.
Amesema gari hilo lilikuwa na abiria Sita ambao ni Naiman Metili, Anjela Metili (36),Colin Mathayo Lyimo (16) ,Lisa Metili (8) ,Brenda Amani (25) ,Martha Metili (40).
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa waliofanikiwa kuokolewa ni Naiman Metil ambaye alikuwa Dereva wa gari hiyo Pamoja na Anjela Metili ambaye kwasasa anapatiwa matibabu katika hospital ya Boma wilayani Hai.
Lakini wengine wote wamefariki ambapo mpaka sasa miili iliyopatikana ni watu watatu huku mtoto Lisa akiendelea kutafutwa kwasababu maji yaliyomsomba yalimpeleka mbali Zaidi
Mheshimiwa Kaganda ametoa wito kwa madereva na watembea kwa miguu kutokuingia katika maji yanayovuka barabara ili kujiepusha na madhara ya mvua kubwa inayonyesha kwa Sasa.
No comments:
Post a Comment