WAZIRI MCHENGERWA ATETA NA WAHIFADHI- TANAPA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 16 April 2023

WAZIRI MCHENGERWA ATETA NA WAHIFADHI- TANAPA

 

Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wafanyakazi WA TANAPA 


Baadhi ya wafanyakazi TANAPA wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii 


Na.Edmund Salaho/ARUSHA

maipacarusha20@gmail.com

Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mohamed Mchengerwa Leo Aprili 16, 2023 ametembelea makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), jijini Arusha lengo likiwa ni kujionea utekelezaji wa shughuli za Uhifadhi na Utalii. Katika ziara hiyo aliongozana na Katibu mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt Hassan Abbasi pamoja na Naibu Katibu mkuu, Anderson Mutatembwa.


Awali, akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA, William Mwakilema, alimshukuru Mhe. Waziri kwa kutenga muda na kuja kuzungumza na watumishi na kupongeza ushirikiano mkubwa ambao shirika limekuwa likipata kutoka  kwa viongozi wa Wizara ili kuifikia adhma ya serikali ya kufikia watalii millioni tano ifikapo 2025. 


Aidha, Kamishna Mwakilema alieleza hali ya mandeleo va miradi va kimkakati va kukuza

utalii na kusema inaendelea vizuri ikiwemo miradi va miundombinu va malazi katika Hifadhi va Taifa Burigi -Chato na Kisiwa cha Rubondo pia miradi ya UVIKO -19  katika Hifadhi va Taifa

Serengeti, Tarangire, Kilimaniaro, Mkomazi, Saadani na Nyerere inayolenga kuboresha miundombinu ya malango ya kuingilia wageni, barabara, na viwanja vya ndege.


Akizungumza na Watumishi hao, Waziri Mchengerwa aliwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuhifadhi na kutangaza vivutio vyetu vya utalii na kuwataka kuongeza juhudi zaidi illi kufikia adhma ya serikali.


“Niwapogeze sana kwa kazi kubwa mnayoifanya katika kuhifadhi na kutangaza vivutio vyetu. Sisi kama viongozi wenu wa wizara idadi ya watalii millioni tano kwetu tunaiona ni ndogo sana nchi yetu ina vivutio vingi na maeneo ya kipekee tukiwa wamoja katika kutangaza idadi ya wageni nchini kwetu itaongezeka sana” alisema Mhe. Mchengerwa


Pia, Mchengerwa alitoa rai kwa watumishi kuongeza nguvu zaidi katika kutangaza vivutio vyetu na kusisitiza mshikamano na nidhamu ya kijeshi na kubainisha

 

“ Tutambue taasisi yetu ni ya kijeshi ni vizuri tukitambua nidhamu ya kijeshi, wanajeshi hatuna kundi lingine sisi kama Jeshi tuna kundi moja tu la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” alisema Mchengerwa.


Waziri Mchegerwa alisistiza kufanya kazi kwa bidii na kuahidi ushirikiano na kusimama na watumishi kwa wakati wote na katika kila hali.

No comments: