MADIWANI KARATU WALIA NA MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday 13 May 2023

MADIWANI KARATU WALIA NA MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO




 NA SOPHIA FUNDI KARATU.


maipacarusha20@gmail.com


Madiwani halmashauri ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha walia na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuacha pori katika eneo lililoko karibu na ofisi zao Jambo ambalo limekuwa kero kwa wananchi  kuvamiwa na wanyama wakali na kuwaua.


Wakizungumza katika  mkutano wa kawaida wa Baraza la madiwani hao walisema kuwa wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi kuhusu pori lililoko kwenye makazi ya watu liliko ofisi za mamlaka ya  hifadhi ya Ngorongoro kuhusu wanyama waliohamia kwenye eneo Hilo na kuwaua wananchi wao.


Diwani wa kata ya Ganako ambaye ni  makamu mwenyekiti wa Halmashauri John Bayyo akichangia hoja amesema kuwa haiwezekani mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuacha pori katikati ya makazi ya watu huku wanyama wakali wakijificha ndani ya pori Hilo na kusababisha vifo kwa wananchi walioko karibu na pori Hilo.


"Mheshimiwa mwenyekiti mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wamekuwa maadui na wananchi kwani tulikaa kikao na kukubaliana pori Hilo kufyekwa lakini Cha kushangaza mpaka leo hakuna kilichofanyika na wananchi wao wanazidi kuuawa na kujeruhiwa na wanyama wakali"amesema diwani huyo.


Naye diwani wa kata ya Gurus Dastan Panga alisema kuwa endapo pori Hilo halitafyekwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wao wataandamana na wananchi wao kufyeka ili kunusuru maisha yao.


Amesema kuwa maeneo ya ofisi za mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro yako kwenye makazi ya watu hivyo ni jukumu la uongozi wa  mamlaka kufyeka msitu uliokuwa  katika ofisi zao.


Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo John Lucian alimwagiza mkurugenzi kuwaandikia barua wamiliki wa mashamba ya mikataba ambayo yamekuwa pori na kuhifadhi wanyama wakali pamoja na  Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kufyeka maeneo hayo ili kuwanusuru wananchi  wao.


*Mkurugenzi tunakuagiza andika barua nyingine kwa wale wote wenye mashamba ambayo yamekuwa pori kuyafyeka mara moja  au kuweka uzio kwani tumechoka kuzika watu wetu na wengine kuachwa vilema wa kudumu*alisema mwenyekiti.


Akihojiwa na mwandishi  naibu kamishna  wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Elibariki  Bajuta amesema kuwa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro inakusudia kuweka uzio katika eneo Hilo ili kuwazuia wanyama wanaodhuru wananchi wa vijiji vya jirani.

No comments: