MTUHUHUMIWA WA UJANGILI ASOMEWA MASHTAKA MAHAKAMANI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 13 May 2023

MTUHUHUMIWA WA UJANGILI ASOMEWA MASHTAKA MAHAKAMANI

 



Mwandishi wetu,Babati


maipacarusha20@gmail.com


Mtuhumiwa wa ujangili wa Twiga katika eneo la hifadhi ya Jamii ya  Wanyamapori Burunge(Burunge WMA) wilayani Babati mkoa wa Manyara Amos Benard Meja Jana amefikishwa  mahakamani kwa tuhuma za uwindaji haramu na upatikanaji wa nyara za serikali.



Mtuhumiwa huyo ambaye alikamatwa april 22 mwaka huu ,kijiji cha vilima vitatu  katika eneo la Burunge WMA  na amefunguliwa Kesi ya uhujumu uchumi namba 7/2023.


Kesi hiyo imetajwa Jana  Mbele ya hakimu mkazi wilaya ya Babati Victor Kimario .


Akimsomea mashitaka hayo, Wakili wa serikali Rose Kayumbo alisema kosa la  Kwanza linalomkabili ni kupatikana na nyara za serikali na kosa ya pili uwindaji haramu wa mnyama twiga.


Alieleza Meja alifanya ujangili wa Twiga April 21 katika eneo la hifadhi ya  Jamii ya wanyamapori ya  Burunge wilaya ya Babati.


 Mtuhumiwa alikana mashitaka hayo na amerudishwa gerezani hadi Mei 5,2023  kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo.,


Mwendesha Mashitaka wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) Getrude Kariongi amesema mtuhumiwa hiyo bado anakabiliwa na mashitaka mengine kadhaa ya ujangili.


"Leo ni Kesi ya Kwanza bado kuna mashitaka mengine ya ujangili tunaandaa atafikishwa  tena mahakamani hivi karibuni "amesema


Amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na mitego ya muda mrefu ambayo ilikuwa imendaliwa na kikosi cha  askari wa Wanyamapori  wa mamlaka ya usimamizi wanyamapori (TAWA) Askari wa Burunge WMA na Askari wa taasisi ya katika chemchem ambao wamewekeza katika eneo hilo.


Meneja wa Chem chem association, Clever Zulu amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo  na kufikishwa mahakamani ni jitihada zilizofanywa na askari wa Wanyamapori.Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya dola Ili kukomesha ujangili katika eneo Hilo.


Zulu amesema askari hao wa Wanyamapori walioongoza kumkamata mtuhumiwa huyo walipata mafunzo maalum kutoka kwa maafisa wa TAWA na Jeshi la Polisi  jinsi ya kufanya upelelezi,upekuzi na ukamataji wa majangili mwezi April mwaka huu.




No comments: